Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza kwenye mkutano wa
hadhara wa wananchi wa kijiji cha Kilangawani kufuatia malalamiko yao
kwa Serikali juu ya Opersheni Tokomeza. Wengi wao walikiri kutegemea
hifadhi ya akiba ya Uwanda kulisha mifugo yao.
Jambo
ambalo wafugaji wameiomba Serikali kuwatafutia maeneo mbadala ya
ufugaji. Kwa upande wao wakulima wameiomba Serikali kuharakisha kutafuta
suluhu ya mifugo inayozagaa vijijini na mashambani baada ya kufukuzwa
kwenye hifadhi kabla ya msimu wa mvua unaokaribia kuanza kwa ajili ya
kilimo kuepusha migogoro kati yao na wafugaji.
Wavuvi
na Wajasiliamali wa samaki waliokuwa wakifanya shughuli zao katika ziwa
Rukwa nao wameiomba Serikali iwape muda wa kuvua angalao wa miezi
mitatu ili waweze kurudisha madeni ya mikopo kutoka taasisi za fedha
walizokopa na kupata nauli za kurudi makwao kwani wengi wao wametoka
maeneo tofauti ya mikoa ya Mbeya, Ruvuma, Njombe na Kilimanjaro.
Sehemu
ya kundi kubwa la Ng'ombe likionekana mitaani kutafuta malisho na maji
katika kijiji cha Maleza katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
Mkoani Rukwa baada ya kufukuzwa katika hifadhi ya akiba ya Uwanda
(Uwanda Game Reserve) ikiwa ni matokeo ya operesheni Tokomeza
inayofanywa na Serikali kunusuru mali asili nchini.
Maeneo yaliyoathirika kutokana na Operesheni Tokomeza yapo katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ambapo zoezi la kuwaondoa majangili na wavamizi wa hifadhi za misitu limegusa vijiji saba (7) vya Ilambo, Maleza, Kilangawana, Mkusi, Kilyamatundu, Nankanga na Msila. Pia wananchi wanaoishi pembezoni mwa Ziwa Rukwa ambapo jumla ya kambi 13 za wavuvi zimechomwa moto.
Inakadiriwa kuwa takribani watu 1600 wameathiriwa na zoezi hili. Aidha, yapo makundi makubwa ya mifugo (ng’ombe) ambayo yamezagaa vijijini na kuna uhaba mkubwa wa chakula kwa familia hizo kutokana na nyumba zao na vyakula kuchomwa moto.

katika kijiji cha Kilangawani katika Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga
Mkoani Rukwa baada ya kufukuzwa katika hifadhi ya akiba ya Uwanda
(Uwanda Game Reserve) ikiwa ni matokeo ya operesheni Tokomeza
inayofanywa na Serikali kunusuru mali asili nchini.
Mkuu
wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella Manyanya akizungumza na moja ya
familia zilizoathirika na Operesheni Tokomeza katika kijiji cha
Kilangawani alipotembelea hivi karibuni kuzungumza na wananchi wa kata
za Kipeta na Mtowisa kufuatia malalamiko yao kwa Serikali juu ya
Opersheni hiyo. Malalamiko hayo ni pamoja na ukosefu wa makazi, vyakula,
maeneo kwa ajili ya wafugaji pamoja na athari nyingine nyingi
zilizosababishwa na Operesheni hiyo. 

Mkuu
wa Wilaya ya Sumbawanga Methew Sedoyyeka akizungumza na moja ya familia
ya wafugaji iliyoathirika na Operesheni hiyo kwa kuharibiwa makazi na
vyakula mbalimbali. Familia hiyo pamoja na nyingine zinazoishi
kandokando ya hifadhi ya akiba ya Uwanda zimekua zikitegemea hifadhi
hiyo inayopakana na Ziwa Rukwa katika kulisha na kunywesha mifugo yao
jambo lililopelekea uharibifu mkubwa wa hifadhi hiyo na ziwa Rukwa kwa
ujumla.
Ndugu
Funuki Kapahungu mfugaji na muathirika wa operesheni hiyo akielezea
operesheni hiyo iliyompitia na kuiomba Serikali kuwatafutia maeneo
mbadala kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao za ufugaji. Hata hivyo
viongozi wa Mkoa wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella
Manyanya waliwashauri wafugaji hao kufuga kisasa ufugaji wenye tija kwa
kupunguza idadi ya mifugo na kuuza mingine kuwawezesha kununua maeneo
madogo ambayo watayaendeleza kwa kuyachimbia visima vya maji na kupanda
nyasi kwa ajili ya mifugo yao. Alisisitizia juu ya uvunaji wa mifugo kwa
kuwawezesha wafugaji kuinuka kiuchumi.
Ndugu
Sadiki Hiari mkazi wa Ilambo akitoa kero zake katika Mkutano huo.
Baadhi ya wananchi wengi walitoa ushauri kwa Serikali ya Wilaya, Kijiji
na wananchi hususani wafugaji kukaa pamoja na kuweka utaratibu maalum wa
kupunguza idadi ya mifugo kulingana na uwezo wa maeneo ya ufugaji
tofauti na ilivyo sasa ambapo mfugaji mmoja ana uwezo wa kufuga ng'ombe
wengi hadi kufikia 10, 000 bila kuwa na utaratibu wa kuwavuna waweze
kuwasaidia kuondokana na umaskini. Wengi wa wafugaji wanaona ufahari
kuwa na mifugo wengi bila hata kujali faida yake kiuchumi.
Uwanja wa Mkutano. Katika Mkutano huu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Stella Manyanya alitoa maagizo na maelekezo mbalimbali yakiwemo Wafugaji waone uwezekano wa
kuvuna mifugo yao ya ziada na kuwekeza katika vitega uchumi vingine mfano
nyumba, mashine n.k. vitakavyowezesha kuendeleza fedha zao. Serikali
zote za vijiji ziainishe
maeneo ambayo bado hayajatumika ili kuweza kuyatengea matumizi bora kwa
ajili
ya mifugo na kilimo na Hiyo izingatiwe kwa
Mkoa wote wa Rukwa. Wavuvi nao waliambiwa kila mwaka kuanzia Januari –
Machi ziwa litafungwa kwa ajili ya kuwezesha samaki kuzaliana na kukua
lakini pia wajizatiti kutumia zana bora za uvuvi. (Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)