CHADEMA YANYAKUA KITI CHA NAIBU MEYA ARUSHA

PictureCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimeshinda uchaguzi mdogo wa kiti cha unaibu Meya wa Jiji la Arusha.

Mgombea wa CHADEMA, Diwani wa Daraja Mbili, Prosper Msofe, alichaguliwa kushika nafasi hiyo, baada ya kupata kura 25, kati ya kura 28, huku mbili zikisema hapana, na moja ikiharibika.

Chama cha Mapinduzi (CCM) hakikusimamisha mgombea, huku TLP yenye Diwani mmoja, Michael Kivuyo aliyetangaza kugombea aliamua kujitoa kabla uchaguzi kufanyika. --- via Lukwangule blog.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo