WATU WASIOFAHAMIKA WAMUUA SEBA ERNEST HUKO MBARALI MBEYA


Na SaimeniMgalula, Mbarali,

Mkazi mmoja Seba Ernest (45) wa kata ya Mahongole Wilayani hapa Mkoani Mbeya,ameuawa kwa kukatwa kichwani na tumboni na vitu vyenye ncha kali na watu wasio fahamika, kisha mwili wake kutupwa mita chache kutoka nyumbani kwake.

Akizungumza kwa uchungu mke wa marehemu Joyce Daniel (39) alisema kuwa waliagana na marehemu majira ya saa mbili usiku akimtaarifu kuwa asubuhi ya octoba 19 mwaka huu atasafiri kuelekea Wilaya ya chunya kwa ajili ya kujenga makaburi.

Aidha imedaiwa baada ya kutoka nyumbani kwa mke mdogo marehemu alipitia kilabuni ambapo watu kadhaa walimuona akitpata kiburudisho .

Baadhi ya majirani walisema kuwa hawakusikia sauti yeyote ya mtu kuomba msaada ingawa ni karibu na makazi ya watu hali iliyosadikika mauji kufanywa eneo nyingine na mwili kutupwa karibu na nyumbani kwake.

Akizungumzia tukio hilo Mwenyekiti wa kijijcha Nsonyanga Asumile Mtawa alisema alipata taarifa kutoka kwa mtendaji wa kijiji ambapo walifika eneo la tukio na kukuta maremu amekatwa kichwa na utumbo ukiwa nje.

Naye Diwani wa kata hiyo Brown Mwakibete alisema kuwa kitendo kilichofanywa na wauaji hao ni cha kinyama ambapo amewataka Wananchi kutoa taarifa jeshi la polisi ili watuhumiwa wakamatwe kujibu tuhuma za mauaji.

Pia mwili wa marehemu ulifanyiwa uchunguzi na Daktari kasha kukabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa mazishi.

Na kwa upande wa kamanda wa polisi mkoa wa mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kutoa wito kwa watu wanao wafahamu walio husika na tukio hilo watoe taarifa polisi ili wakamatwe na kuchukuliwa hatua za kisheria.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo