Meneja
Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu na Majini (SUMATRA)
Bw. David Mziray akitoa wito kwa wamiliki wa Pikipiki na madereva wa usafiri
huo kushirikiana katika kuhakikisha wanatekeleza sheria na kanuni zilizowekwa
na Mamlaka hiyo, wakati wa Mkutano uliofanyika ukumbi wa Idara ya
Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO
Mkurugenzi
Udhibiti wa Usafiri Barabarani kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu
na Majini (SUMATRA) Gilliard Ngewe akieleza kwa waandishi wa Habari(hawapo
pichani) juu ya Kanuni za Kudhibiti Usafiri wa Pikipiki na Bajaj, wakati wa Mkutano
uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia
ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bi.Fatma Salum.
Mkurugenzi
Udhibiti wa Usafiri Barabarani kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Nchi Kavu
na Majini (SUMATRA) Gilliard Ngewe akieleza kwa waandishi wa Habari(hawapo
pichani) juu ya Kanuni za Kudhibiti Usafiri wa Pikipiki na Bajaj, wakati wa Mkutano
uliofanyika ukumbi wa Idara ya Habari(MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kulia
ni Afisa Habari wa Idara ya Habari Bi.Fatma Salum.
========= ======= ======
Mamlaka ya
udhibiti usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA) imewataka wamiliki na
madereva wa pikipiki na Bajaji kufuaata na kuzingatia sheria na kanuni za
usafirishaji.
Wito huo
umetolewa na Mkurugenzi wa Udhibiti wa Usafiri wa barabara Gilliard Ngewe wakati
wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Ngewe
amewataka wamiliki na waendesha vyombo hivi
kuzingatia wajibu wao kwa
kujiwekea mfumo wa udhibiti wa ndani wa kuhakikisha wanaheshimu sheria, na
kudhibiti vitendo vyote vya uvunjaji wa sheria na kulinda usalama wao na abiria
wao.
Aliongeza
kuwa ni vyema wamiliki wakatambua masharti ya Leseni zao ambayo aliyataja kuwa
ni kwanza pikipiki husika kutoa huduma katika eneo lililoruhusiwa kwa mujibu wa
sheria na lazima pikipiki husika zikidhi viwango vya shirika la viwango. Alifafanua
zaidi kuwa dereva wa pikipiki haruhuswii kubeba abiria zaidi ya mmoja ambapo
kwa pikipiki za miguu mitatu zinatakiwa kubeba abiria kama inavyotakiwa kwa
mujibu wa leseni zao zinazowapa kibali cha kubeba abiria wasiozidi watatu.
Pia Dereva
wa pikipiki anatakiwa kuvaa kofia ya kujikinga na kuwa na alama ya eneo
analofanyia biashara ya kubeba abiria.
Ngewe alisema Ngewe
aliongeza kuwa abiria wanatakiwa kuvaa kofia ya kujikinga wakati wote
wanapotumia usafiri wa
huo ili
kuepusha madhara yanayoweza kuwapata
mara ajali inapotokea.
Naye Meneja
mawasiliano wa Mamlaka hiyo David Mziray
alisema wanashirikiana na mamlaka nyingine
kama halmashauri za miji na
polisi katika kuhakikisha kuwa sheria na
kanuni za usafirishaji zilizowekwa zinazingatiwa.
Sumatra imewataka wamiliki na waendeshaji wa vyombo hivi kujiwekea mfumo wa
udhibiti wa ndani na kuhakikisha wanadhibiti vitendo vya kihuni na kulinda
usalama wao wenyewe na abiria.


