NAY WA MITEGO ATUPWA LOKAPU KWA KOSA LA KUVAA SARE ZA POLISI


Rapper Ney Wa Mitego ameniambia kuwa hii picha hapo juu tukio hilo limetokea Jana wakati wana shoot video ya wimbo wake Unaofanya vizuri kwa sasa kwenye radio stations ' Salam Zao'.


Ney Wa Mitego Amesema ' Nikweli nilitupwa sero jana baada ya raia wasio julikana kuleta fujo eneo la kazi yangu  kwasababu kulikuwa na waigizaji waliokuwa na sare za polisi. Watu hao sijuani nao na walijitambulisha kama askari na kutaka kujua kwanini natumia sare za polisi kwenye video yangu bila kibali. hicho ndio kitu kilichopelekea nikapelekwa polisi.

Mitego ameendela kusema kuwa baada ya kuka sero kwa dakika kama 15 mkuu wa kituo alikuja na kusikiliza tatizo hilo na ndio aliachiwa huru baada ya kutoa maelezo kuhusu tukio hilo na sare hizo kuonekana uraiani.

Ney aliwekwa sero Kwenye kituo cha polisi Urafiki kilichopo Manzese na wiki ijayo video hii itaonekana kwenye vituo vya televison Tanzania.


CHANZO:SAMMISAGO.COM


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo