RAIS KIKWETE AWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU MANUFAA YA GESI

 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgfvy6LdDRUYNWrw6yqkE2jpCcaMwsG7AtRkHQmYQIS1ZdvY7Of-5kH8DRDK2Wgu2iRZJexHbdDHVVT6DdAl3Isl_ISgplS2qnBtSKLObw3eTVCqGymH9SHr_kcReRixpq6N66I1pkVUWu7/s1600/D92A8783.jpg
Rais Jakaya Kikwete amewatoa  wasiwasi Watanzania wanaodhani kuwa mchakato unaoendelea sasa  kuhusu mafuta na gesi hautawanufaisha na badala yake amesema serikali imejipanga vyema kuhakikisha  taifa linanufaika na rasilimali hizo.
 
Mh Rais ameyasema hayo katika uzinduzi wa awamu ya nne ya ufunguaji wa zabuni za  vitalu vya utafutaji wa leseni za utafutwaji wa gesi na mafutra nchini. 

Aidha Mh Rais amesema anatambua mawazo mazuri yanayotolewa ya kuwashirikisha sekta binafsi Ili kuweza  nao kushiriki katika mchakato huo wa mafuta na gesi.

Pia kiongozi huyo mkuu wa nchi akaongeza kuwa kwa sasa serikali inachofanya ni kuhakikisha kuwa inajenga uwezo wa kufanya ukaguzi wa kina katika maeneo ambayo gesi .

Naye waziri wa nishati na madini Mh Profesa Sospeter Muhongo  amesema sera ya gaesi na mafuta Ipo tayari na kichofanyika sasa ni kuiandika katika lugha ya Kiswahili.

Nao baadhi ya wabunge na wadau mbalimbvali walioshiriki katika mkutano huo wamesema imekuwa jambo jema kwa rais kutoa ufafanuzi wa jambo hilo kwa kina kutokana na ukweli kuwa watu wengi walianza kuwa na wasi wasi kuwa taifa linapata hasara.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo