MWILI WA MAREHEMU KAMANDA KOMBE KUAGWA IJUMAA HII

Marehemu James Kombe
Marehemu James Kombe.
Na Frank Geogrey, Jeshi la Polisi

Mwili wa aliyekuwa Kamanda Mstaafu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kamishina Msaidizi Mwandamizi (SACP) James Kombe utaagwa Ijumaa katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania lililopo Usharika wa Msasani jijini Dar es salaam.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa kamati ya mazishi inayojumuisha Familia ya marehemu na Jeshi la Polisi Naibu Kamishina wa Polisi (DCP) Thobias Andengenye.

Aliongeza kuwa ndugu, jamaa, marafiki maofisa wa polisi, askari pamoja na viongozi mbalimbali watapata fursa ya kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu na baadae mwili utasafirishwa kuelekea Moshi, mkoani kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.

James Kombe alifariki dunia Oktoba 22 mwaka huu wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Ocean Road jijini Dar es Salaam, Kombe alizaliwa mwaka 1950 huko Mwika mkoani Kilimanjaro na alijiunga na Jeshi la Polisi tarehe 15 mwezi machi mwaka 1970 baada ya kuhitimu elimu ya sekondari mwaka 1969 nchini Uganda ambapo alipandishwa vyeo na kupewa madaraka mbalimbali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo