Siku moja baada ya Boss wa Watanashati Ostaz Juma na Musoma
kutangaza kuwa amemfukuza Janjaro kwenye kundi la watanashati kwa sababu
za utovu wa nidhamu, C.E.O huyo ameamua kumrudisha tena kundini rapper
huyo.
Ostaz Juma ameiambia tovuti ya Times fm exclusively kuwa ameamua
kumrudisha kundini Janjaro kwa kuwa ameonesha hali ya kuelewa na
kumhakikishia kwamba amebadilika.
“Nimeamua kumrudisha, kwa sababu yale mambo yaliyopelekea mpaka mimi
kutoa maamuzi yale niliyotoa jana, yaani kawa kama mtu mzima mwenye
akili timamu, na mtu yeyote anayelifikiria na akaona kwamba hili ni kosa
akasema kwamba ntajirudi, ni kumpa nafasi ya kumsikiliza.
“Kwa hiyo jana tulikaa kama kikao cha familia nyumbani kwangu,
tukazungumza na ni kweli ameona kwamba ni bora aache baadhi ya mambo
ambayo hayakuwa mazuri kwenye jamii, na mimi nachokitaka dogo Janja awe
mtu bora, awe mzuri katika jamii.
Na yeye ameniahidi kwamba,
atawahakikishia watanzania kwamba atakuwa dogo janja ambae watanzania
wanamtaka wao.” Amesema Ostaz Juma.
Janjaro ameiambia tovuti hii kuwa bado yuko watanashati na kwamba ile tofauti kati yao ilimalizika baada ya kikao.
“ Mi niko mtanashati, kwa sababu ni mambo ya kifamilia na tumeshakuwa
familia moja, na mimi naona kuhamahama sio swala zuri, na kama nilikuwa
na malengo ya kufanya kazi nzuri, ni bora niendelee kupalilia tu
hapahapa. Yamekwisha isha kwa ufupi.”
Kuhusu wapi alikosea na anaona hatakiwi kurudia tena,janjaro amewatupia lawama 'marafiki' kwa kuwa chanzo cha yote.
“Kwa namna moja ama nyingine ni ile chuki, marafiki ambao wamenizunguka, ni watu ambao ni soo, sio watu wazuri. Sasa hivi rafiki yangu hela tu.”
Janjaro na Ostaz Juma kwa pamoja wameahidi kuendelea kutoa burudani
kwa fans wao,ambapo Ostaz amesema sasa hivi amejipanga zaidi kama msanii
na ataachia ngoma nyingi kali akiwa na wasanii wengine wa kundi la
Watanashati.
