Zaidi ya wanaume 100,000 katika Wilaya ya Baridi mkoani Simiyu,
wanatarajiwa kufanyiwa huduma ya tohara, ndani ya kipindi cha miaka
mitano katika mradi wa tohara kwa wanaume wilayani humo ulioko chini ya
shirika lisilo la kiserikali Intra Health kwa kushirikiana na serikali.
Mradi huo ambao uko chini ya shilika hilo linalojishugulisha na utoaji huduma za afya kwa jamii unalenga kuwafikia wanaume 127,840, kwa kipindi cha miaka mitano,na idadi hiyo ya wanaume ni kuanzia umri wa miaka 10 hadi 30.
Hayo yalibainishwa jana na Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Dk Asey John katika ufunguzi wa kituo cha kutolea huduma hiyo katika hospitali ya wilaya, ufunguzi uliofanya na Mwenge wa uhuru unaokimbizwa katika wilaya hiyo.
Asey alisema kuwa mradi huo ulianza mwaka 2010 ambapo mpaka sasa una mika 3 tangu uanzishwe na unatalajiwa kufikia mwisho wake mwaka 2015 ukiwa umefikisha miaka mitano.
Aliongeza kuwa katika ujenzi wa kituo hicho kiasi cha shilingi Milioni 58,433,040 zimetukika kufanikiwa kujenga kituo hicho, fedha kutoka kwa shirika hilo la Intra Health kwa kushirikiana na serikali, lengo kubwa likiwa ni kupunguza maambukizi ya Virusi vya UKIMWI kwa asilimi 60.
Alibainisha kuwa tangu kuazisha kwa mradi huo jumla ya wanaume 27,969 kutoka mwaka 2010 hadi julai mwaka huu 2013 wameishapatiwa hudumua hiyo, huku akibainisha changamoto mbalimbali ambazo wamekutana nazo kuwa kukosekana kwa elimu kwa wanaume juu ya umuhimu wa huduma hiyo.
Aliongeza changamoto nyingine ni kuwepo kwa imani potofu kwa baadhi ya wanaume kuwa kufanya tohara kunasababisha kuwepo kwa ugumba, pamoja na wanaume wengine ambao wamekuwa wakipata huduma hiyo kutokuzingatia usafi hali inayowasababishia matatizo mengi.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Juma Ali Simai aliwaka waname kujitokeza kwa wingi kupata huduma hiyo, sambamba na kuwataka kuachana na imani hizo potofu, huku akiwasisitiza wanawake kuwashawishi waume zao kwenda kupata huduma hiyo.
Sambamba na hayo mwenge huo wa uhuru ulizindua kituo cha Kilimo na ufugaji katika kata ya Dutwa, kilichojengwa na mpango wa maendeleo ya kilimo wilaya DADIP kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya hiyo pamoja na wananchi,kikiwa kimegharimu kiasi cha shilingi Milioni 47,209,190.
Akisoma taarifa ya kituo hicho kwa kiongozi wa mwenge kitaifa Mtendaji wa kata hiyo Kasili Mabula alisema kuwa kituo hicho kitaweza kuhudumia zaidi ya wakulima pamoja na wafugaji 800, ikiwa ni asilimia 50 ya wananchi wote katika kata hiyo, ambapo wataweza kupata elimu juu ya kilimo bora pamoja na ufugaji wa kisasa.

CHANZO:habarimasai.com