MAPIGANO KATI YA WAFUGAJI WA KIMASAI NA WABARBAI YAUA WAWILI MOROGORO


 Watu wawili wameuwa  baada ya kuzuka mapigano  kati wafugaji  jamii ya Wamasai  na Wabarbai katika vijiji vya  Mtibwa wilayani Mvomero Mkoani Morogoro.
 
Mapigano hayo yamekuja kufutia ugomvi  uliozuka kutokana na kugombania maeneo ya malisho  ambapo wakielezea tukio hilo wafugaji wa jamii ya wabarbai wamesema chanzo ni mkulima mmoja kuuza  shamba la  malisho kwa wafugaji wawili  hali iliyozua kutokuelewana baada ya wafugaji kujikuta wakilisha mifugo katika shamba moja ndipo  ulipozuka ugomvi na mapigano  na kuuwawamfugaji mmoja jamii ya  Mbarbai na baadaye wakalipiza kisasa kwa kuumua mfugaji  wa kimasai.
 
Kufutia  mapigano hayo  serikali ya wilaya  na Kamati ya Ulinzi  na Usalama walilazimika kufanya mikutano kwa makundi hayo ya wafugaji   ambapo mkuu wa   Wilaya ya Mvomero Antony Mtaka  amesema  serikali    itawakamata waliohusika  na mauaji ya wafugaji hao huku akiwataka wafugaji wavamizi wa mashamba  kuondoka ndani ya siku saba katika maeneo hayo ambayo si  rasmi kwa shughuli za ufugaji.
 
Katika tukio jingine  watu wasiofahamika  wamemuuwa kikatili mfugaji  mmoja jamii ya wamasai  mkazi wa kijiji cha Twatwatwa  wilaya ya Kilosa   na kuzikwa nusu  katika mashamba ya mkonge  ambapo wananchi wameomba serikali kutafuta waliohusika na tukio hilo huku kamanda wa polisi Mkoa wa Morogoro Faustine Shilogile amesema uchunguzi unaendelea na baadhi ya watu wanashikiliwa kuhusika na mauaji hayo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo