MWENGE WA UHURU WATUA MKOANI PWANI

Mwenge wa Uhuru ukiwa mpakani mwa Mkoa wa Morogoro na Pwani leo tayari kwa makabidhiano ya Mwenge huo uliomaliza ziara yake mkoani morogoro na Kuanza ziara Mkoa wa Pwani mara baada ya kutembelea wilaya zote za mkoa wa morogoro kwa lengo la kukagua na kufungua miradi na shuguli za Maendeleo Mkoani Morogoro.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro na Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mh Innocent Kalogeris wakati wa Shamra shamra za Mbio za Mwenge wa Uhuru uliomaliza ziara yake Mkoani Morogoro Leo.
Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Morogoro wakiwa katika makabidhiano hayo leo.
Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Pwani wakiwa katika Mapokezi hayo leo
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Mh Joel Bendera  akikabidhi mwenge wa Uhuru kwa Mkuu wa mkoa wa Pwani Mh Mwamtumu Mahiza leo mara baada ya mwenge huo kumaliza ziara yake mkoa wa morogoro
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mh Mwamtumu Mahiza akipokea Mwenge wa Uhuru 
Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Na Mbunge wa Jimbo la Bagamoyo Mh Dk Shukuru Kawambwa  akiwa na Naibu Waziri wa Afya Seif S Rashid wakiwa katika Mapokezi hayo..


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo