Kinachoning'inia kwenye hiyo transfoma kinasadikiwa ni bomu... Taarifa ambazo zimetufikia hivi punde kutoka kijitonyama jijini Dar es
salaam zinasema kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania usharika wa
Kijitonyama limenusurika kulipuliwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni bomu
jioni hii baada ya watu wasiojulikana kutupa box lililofungwa huku ndani
likiwa na kitu kinachodhaniwa kuwa ni wakati shughuli
mbalimbali zikiwa zinaendelea.
shuhuda wetu kutoka eneo la tukio
anasema box hilo limetupwa karibu kabisa na Transfoma ya TANESCO iliyopo
ndani ya eneo la kanisa hilo.
wakati Tukio hilo likitokea
shughuli mbali mbali zilikua zikiendelea kanisani humo ikiwa ni pamoja
na mazoezi ya kwaya,Fellowship na maombezi ambapo waumini hao
walistushwa na utupwaji wa box hilo kitendo kilichozua tafrani kubwa na
kulazimika kuwasiliana na vyombo vya ulinzi na usalama ambapo vilifika
eneo la tukio muda mfupi na kulichukua box hilo huku wakiwazuia
waandishi wa habari kupiga picha box hilo.
Hata hivyo taarifa zinasema hakuna mtu yoyote ambaye amedhurika katika tukio hilo.
|