NAIBU WAZIRI WA UJENZI GERSON LWENGE AFANYA ZIARA KIJIJI CHA KIDUGALA MKOANI NJOMBE

 Wananchi wa Kijiji Kipya cha Kidugala wakiwa Juu ya TANURI la Tofari wakimsikiliza Mbunge wao(Picha zote na Gabriel Kilamlya)
 Naibu Waziri wa Ujenzi Mhandisi Gerson Lwenge akiweka Jiwe la Msingi Kwenye Ujenzi wa Ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Kidugala wakati wa Ziara yake Jimboni Humo.

 Mbunge wa Jimbo la Njombe Magharibi Mhandisi Gerson Lwenge akikagua Ujenzi wa Ofisi ya Kijiji Kipya cha Kidugala wakati wa
Ziara yake Jimboni Humo.
 Naibu waziri wa Ujenzi akikagua Ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Kidugala.



Milioni 1.1 zatolewa na Mbunge huyo kusaidia Ujenzi wa Ofiisi hiyo na Ukarabati wa Shule.

Wananchi wa Kijiji cha Kidugala wamelazimika Kuweka Mkutano wa Mbunge wao Gerson Lwenge Kwenye Shughuli za Ujenzi wa Ofisi ili atambue Shughuli wanazo zifanya katika Kijiji chao.

Wananchi Hao wamefanya Hivyo ili kumshawishi Mbunge Huyo kuguswa na Ujenzi wa Ofisi hiyo ya Kijiji kipya Cha Kidugala Wilayani Wanging'ombe Ili aweze kuchangia chochote ambapo naye akalazimika Kuchangia Shilingi Milioni 1.1

Hii ni Katika Kuhitimisha Ziara yake ya Juma zima Jimboni Kwake Njombe Magharibi Mbunge Gerson Lwenge ambaye Amefanya ziara ya Kuwatembelea wananchi wake na Kisha Kuchochea shughuli za Maendeleo wanazo zifanya.
 
NA GABRIEL KILAMLYA


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo