Baadhi
ya maofisa wa Ikulu wakiongozwa na aliyekuwa Katibu Mkuu
Kiongozi, Philemoni Luhanjo (wa kwanza kushoto) wakiwa na sura za
huzuni wakati wakiusubiri mwili wa marehemu Timoth Apiyo.
…Luhanjo akiambiwa jambo na mmoja wa wataalamu wa masuala ya Itifaki.
… Baadhi ya waombolezaji waliofika kuupokea mwili huo kama wanavyoonekana pichani.
…
Mkuu wa Wilaya ya Kionondoni, Jordan Lugimbana (wanne toka kulia) akiwa
na baadhi ya maofisa wakati mwili ukitolewa ndani kuletwa nje ya uwanja
wa ndege.
…Mwili wa marehemu Apiyo ukipokelewa.
… Ukiombewa na waombolezaji.
… Ukiingizwa kwenye gari maalum ili upelekwe nyumbani kwake Sitakishari.
… Mwili ukiingizwa nyumbani Sitakishari.
…Waombolezaji wakilia mara baada ya mwili wa marehemu kufika nyumbani Sitakishari.
Ilikuwa ni simanzi kubwa ndani ya famila ya marehemu Timoth Apiyo
pamoja na marafiki na viongozi wa serikali baada ya mwili wa katibu mkuu
kiongozi mstaafu wa Ikulu kuwasili nchini ukitokea Afrika Kusini na
kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere saa moja usiku jana .
Apiyo alikuwa katibu mkuu kiongozi enzi ya utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius Nyerere.
Katika mapokezi hayo, mkuu wa Itifaki kwenye mapokezi hayo ni
aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi Ikulu Philemon Luhanjo na mara baada ya
kupokelewa mwili ulipelekwa nyumbani kwake Sitakishari, jijini Dar
ambapo leo utaagwa katika Viwanja vya Karemjee na inatarajiwa Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, Dk. Mohammed Bilal ndiye
atakayeongoza zoezi hilo.
Baadaye mwili huo utapelekwa kuzikwa kwao kijijini Marasibora wilayani Tarime, Mkoa wa Mara.
PICHA, HABARI NA HARUNI SANCHAWA GPL
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi