Rais wa zamani wa Afrika Kusini Mzee Nelson Mandela amelazwa tena hospitali kutokana na kujirudia tena kwa ugonjwa wa mapafu.
Afya
ya Mandela mwenye umri wa miaka 94 ilianza kudhoofika na kubidi
kupelekwa katika hospitali mjini Pretoria, ambapo taarifa zimesema yuko
katika hali mbaya lakini imara.
Msemaji wa rais nchini humo Mac Maharaj amekaririwa akisema baadhi ya wanafamilia wake wamekuwa na karibu muda wote.
Amesema ni hali ambayo amekuwa nayo kwa kipindi kirefu na wanamatumaini kuwa na sasa pia itatibika kwa mafanikio.
Katika
taarifa yake kutoka ikulu amesema rais huyo wa zamani yuko chini ya
uangalizi wa madaktari bingwa ambayo wananya kila liwezekanalo
kuhakikisha anapata nafuu na kurejea katika hali ya kawaida.
Taarifa hiyo ya ikulu imeongeza kuwa Rais Jacob Zuma kwa niaba ya Serikali na taifa anamuombea Madiba apone haraka