skip to main |
skip to sidebar
WAZIRI SITA AIPONDA RASIMU YA KATIBA MPYA
Waziri
wa ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samweli Sitta amesema mchakato
wa rasimu ya katiba mpya iliyotangazwa imelenga kuwatafutia ulaji
viongozi wa serikali na kwamba inahitajika kufanyiwa kazi ya ziada na
kudai kuwa muungano au shirikisho haviwezi kupatikana kama vipengele
vinavyohusu serikali ya Tanzania bara havijaelezwa vizuri.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam kwenye mahafali
ya chuo cha Ualimu Kibamba Mh Sitta amesema endapo kutakuwepo na rais wa Tanganyika ina maana nchi itakuwa kihoja kwa kuwa na marais watatu na
kueleza kuwa kama yakipitishwa basi wananchi wakubali kuwepo na mzigo wa
kuwahudumia na hata itifaki yake itakuwa ni tabu na kudai kuwa rasimu
hiyo ni dhahiri viongozi wanajitafutia ulaji ndani ya katiba mpya kwani
haelewi ni kwanini tume imependekeza mawaziri 15 wakati masuala ya
muungano yapo saba
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi