Mwanaume mmoja, amepewa onyo na polisi baada kitendo alichofanya, cha
kupiga simu katika namba ya dharura ya 999 kulalamika kwa polisi kuhusu
mvuto wa kahaba aliyemuajiri kwa kupitia simu.
Polisi wa mji wa Midland, nchini Uingereza wamesema walipigiwa simu na jamaa huyo ambaye alisema “nataka kuripoti uvunjaji wa mkataba wa mauzo,” akilalamika kwamba kahaba aliyemuajiri kwa njia ya simu, hakuwa mzuri na wala hana mvuto kama alivyojielezea wakati wakijadiliana bei kwa njia ya simu.
“Mpiga simu amedai kwamba wakati wakiongea kwa simu kabla ya kukutana, kahaba huyo alikuza uzuri na mvuto wake; mvuto wake si kama alivyojielezea kwenye simu hivyo amevunja mkataba wa mauzo.” Msemaji wa polisi amesema.
Katika simu hiyo kati yake na polisi, mwanaume huyo anasikika akisema: “Tulipanga kukutana lakini kabla ya hapo, nilimuambia anieleze kiukweli kuhusu mvuto wake, ama sivyo sitafanya naye biashara tukikutana”
“Kwa kifupi amedangaya; ametoa maelezo ya uongo kuhusu mvuto wake. Tulivyokutana nikamueleza ukweli, akapandwa na hasira” alisema bwana huyo.

Jamaa huyo hadhani kuwa amefanya kosa lolote, na mwenye hatia ni kahaba huyo; kitu cha kushangaza sababu ni kinyume cha sheria ya sehemu hiyo kununua ngono.
Jeshi la polisi la mji huo, limemtumia barua rasmi mwanaume huyo kumuonya kuhusu kuwapotezea muda polisi