WATEJA KUELIMISHWA KUTUMIA M-PESA KUPUNGUZA GHARAMA ZA MAISHA

Meneja Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanzania, Salum Mwalim (kulia) akielezea kwa waandishi wa habari huduma ya M-pesa benki popote inayowaunganisha wateja wa Benki ya Amana na nyingine mbalimbali nchini kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti kwa njia ya M-pesa wakati wa zoezi la kuwaelimisha wateja wa benki hiyo tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Kaimu Meneja wa Tawi hilo Khamis Gumbo.
Meneja wa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanzania Salum Mwalim akifafanua jambo kwa mteja wa Benki ya Amana Tawi la Kariakoo Suleiman Mahmud kuhusu huduma ya M-pesa Benki popote inayowapa uwezo wateja wa Amana kuweka na kutoa fedha katika akaunti zao kwa njia ya M-pesa. Kushoto ni Meneja Masoko wa Benki ya Amana Fatma Mruma na Kaimu Meneja Tawi la Kariakoo Khamis Gumbo. Vodacom imeanza kampeni ya kuwaelimisha wateja namna ya kunufaika na huduma ya M-pesa benki popote inayopatikana kwenye benki mbalimbali za biashara hapa nchini.
Mteja wa Benki ya Amana Suleiman Mahmud akielezea namna anavyoifahamu huduma ya kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti ya Benki hiyo kwa njia ya M-pesa wakati wa zoezi la kuelimisha wateja kuhusu huduma ya M-pesa  benki popote iliyofanyika katika Tawi la Kariakoo jijini Dar es Salaam. Wanaomsikiliza ni Meneja wa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanznaia Salum Mwalim (wa kwanza kulia), Meneja Masoko wa Benki ya Amana Fatma Mruma (wa Kwanza kushoto) na Kaimu Meneja wa Tawi hilo Khamis Gumbo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo