Jengo la ofisi za Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gelard Guninita akisoma taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Wilaya hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu, January hadi April mwaka huu 2013.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo
Mohamed Ngwalima (mwenye upara) kiwa na wakuu wa idara pamoja na kamati
ya ulinzi na usalama katika kikao cha taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Wilaya hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu, January hadi April mwaka huu 2013.
Viongozi wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Kilolo wakifuatilia kwa umakini taarifa.
Mkuu wa idara akisikiliza kwa umakini taarifa hiyo.
Na Oliver Motto
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa inataraji kutumia shilingi Bilioni sita arobaini
na tatu milioni laki tatu themanini na mbili elfu, miambili sitini na tatu na
senti kumi na tano(6,043,382,263.15/=) katika
kipindi cha fedha cha mwaka 2013/2014.
Hayo
yamezungumzwa na mkuu wa Wilaya ya Kilolo Gelard Guninita wakati akisoma
taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika Wilaya hiyo kwa kipindi
cha miezi mitatu, January hadi April mwaka huu 2013.
Guninita
amesema licha ya fedha hizo pia Wilaya iliidhinishiwa bakaa ya Sh.Bilioni 1.1 ( 1,111,039,582.33) fedha ya mwaka 2011/2012 kwa ajili ya
utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo.
Aidha
Guninita amesema hadi kufikia mwezi April 2013 Halmashauri ya Wilaya ya kilolo
imepokea zaidi ya shs Bilioni 4. (4,136,213,628.63)
ikijumuishwa na bakaa ya mwaka 2011/2012.
Amesema
Jumla ya shs. Bilioni 2.4 (2,489,306,451.99) zilizotumika
kwa kipindi cha Julai hadi April, 2013 Kwa
ajili ya utekelezaji wa miradi
mbalimbali ya maendeleo.