Mkurugenzi
wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John
(kushoto) akimwelezea Katibu Mkuu kutoka wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda kuhusu picha ya kinyago
kinachoonyesha mtawala wa makabila mbalimbali ya nchi hiyo
alipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Jumla ya
wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria
wako nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano.
Katibu
Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda
(kulia) akimkabidhi picha ya wamasai Mkurugenzi wa kikosi cha Maji
kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) wakati wanajeshi
22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipomtembelea ofisini kwake
leo jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Sethi Kamuhanda
(kulia) akimkabidhi picha ya kinyago cha ujamaa Mkurugenzi wa kikosi
cha Maji kutoka nchini Nigeria Meja Generali Ati John (kushoto) wakati
wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu walipomtembelea
ofisini kwake leo jijini Dar es Salaam. Wanajeshi hao kutoka nchini
Nigeria wako ziara ya mafunzo ya siku tano nchini.
Kanali
Anderson Msuya (kushoto) kutoka Jeshi la Wananchi la wa Tanzania (JWTZ)
akiongea jambo na Mkurugenzi wa kikosi cha Maji kutoka nchini Nigeria
Meja Generali Ati John wakati wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na
Unadhimu walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Mchezo
leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza Joyce Fisoo akielezea kuhusu
kazi za bodi hiyo kwa wanajeshi 22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu
cha nchini Nigeria walipoitembelea wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni
na Michezo leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Joyce Hagu ambaye ni Kaimu
Mkurugenzi msaidizi Idara ya utamaduni.
Wanajeshi
22 kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu cha nchini Nigeria wakiwa
katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo wakati walipoitembelea wizara hiyo leo jijini Dar
es Salaam. Wanajeshi hao kutoka chuo cha Ukamanda na Unadhimu wako
nchini kwa ziara ya mafunzo ya siku tano.