Serikali
imetangaza kufunga machimbo ya Moram yaliyopo eneo la Moshono jijini
Arusha mpaka itakapoweka utaratibu mzuri wa uchimbaji katika eneo hilo.
Waziri Mkuu nchini, Mizengo Pinda ametoa agizo hilo LEO baada ya kufanya ya kutembelea eneo hilo sanjari na kuwajulia hali majeruhi wawili walionusurika katika tukio hilo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.
Waziri Mkuu nchini, Mizengo Pinda ametoa agizo hilo LEO baada ya kufanya ya kutembelea eneo hilo sanjari na kuwajulia hali majeruhi wawili walionusurika katika tukio hilo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa ya Mount Meru.
Pinda amefika LEO jijini Arusha majira ya mchana na kupokelewa na viongozi balimbali na kwenda moja kwa moja katika Hospitali ya Mt. Meru kuwatembelea majeruhi walionusurika katika ajali hiyo.
Katika hospitali hiyo Waziri Mkuu alishuhudia maiti 14 ambazo zilifukiwa na kifusi cha Moram na kutoa salamu za pole kwa ndugu wa wafiwa.
Baada ya kutoa salamu za pole kwa ndugu wa wafiwa msafara wa Waziri Mkuu ulielekea moja kwa moja katika eneo la tukio na kuona kifusi kilichowafukia watu hao na kusababisha kupoteza maisha.
Awali Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Stephen Masele ameueleza umma kwamba baadhi ya viongozi wa serikali na Halmashauri ya Jiji la Arusha kwamba wana tabia kuchukua mapato katika machimbo hayo badala ya kuangalia usalama kwanza wa wananchi.
“Viongozi wote wa serikali hapa Arusha pamoja na halmashauri ya jiji tusimamie usalama wa Watanzania kabla ya kukimbilia kupokea mapato,”amesema Masele.