Huyu ni mtoto wa Nane wa Marehemu
bwana Carlos Mlowe ambaye amesema hakubaliani na utenguzi huo na kwamba
wamelazimishwa kuzika eneo ambalo sio lenyewe.
Na Gabriel Kilamlya
Mvutano wa kifamilia juu ya eneo la
Kumzika baba mzazi umeibuka katika kijiji cha Mfereke Kata ta Utalingolo
Wilayani Njombe kufuatia baadhi ya ndugu wakionekana kupingana na
wengine kwa kile kinachodaiwa kutengua uamuzi wasia wa marehemu juu ya
eneo la Kuzikwa.
Mvutano huo umekuja kufuatia eneo lililotajwa kuzikwa kwa marehemu Damian Mlowe mwenye umri wa miaka 100 Mkazi wa Mfereke Njombe kuchukuliwa na wawekezaji wa Kanisa Katholiki ambao walishalipa fidia ya mali zilizokuwemo kwen ye eneo hilo la takribani ekari mbili ambavyo ni Vitindi.
Wakizungumza na kituo hiki baadhi ya watoto wa Marehemu akiwemo mtoto wa kwanza bwana Benedict Damian Mlowe na mtoto wa Nane bwana Carlos Mlowe wamesema kuwa hali hiyo imejitokeza kufuatia kutengua maamuzi ya marehemu juu ya eneo la kumzika na hivyo wawekezaji hao kudai kuwa hata makaburi yaliyopo yanatakiwa kuhamishwa na hivyo hakuna sababu ya kuzika tena eneo hilo.

Eneo hilo la Takribani ekari Mbili limetajwa kutolewa fidia ya bati 30 za nyumba ya Marehemu katika kanisa Katholiki Njombe akitoa fursa ya kimaendeleo kwa kujenga chuo cha Mfereke
Maelezo ya mtoto wa marehemu wa tatu ambaye alikuwepo kwenye utoaji wa maamuzi baina ya uongozi wa Kanisa katholiki bwana Sevelina Mlowe amesema malalamiko hayo ni ya baini ya watu wachache bali kushirikishana.
Mwenyekiti wa Kijiji hicho bwana Alex Ngole na afisa mtendaji wa Kata hiyo bwana Stanley Mgohele ambaye awali alikuwa afisa mtendaji wa kijiji hicho wamekana kupokea malalamiko ya mvutano huo ikiwa baadhi ya ndugu kuridhia baba yao kuzikwa eneo jingine Lililopo kanisani na ndiko walikozika.