MWANDISHI wa Kampuni ya Tanzania
Standard Newspapers (TSN) Limited inayochapisha magazeti ya Habari Leo,
Daily News, na SpotiLeo, Peter Temba amevamiwa nyumbani kwake na watu
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, usiku wa kuamkia Aprili mosi mwaka huu.
Temba anayeandikia gazeti la Daily News
mkoani Kilimanjaro, alisema alivamiwa saa 7:30 usiku katika kibanda
chake cha kuuzia vinywaji na chakula kilichopo nyumbani kwake Rau
Madukani wilaya ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Hali hiyo ilisababisha dereva aliyekuwa
akiendesha gari hilo kuliwasha na kukimbia huku akiwaacha wenzake
wawili. Alisema wananchi walijitokeza na kukamata mtu mmoja kati ya hao
na kumshambulia kwa silaha mbalimbali.
Polisi waliwasili eneo la tukio na kumnusuru mtuhumiwa huyo.
Alikimbizwa hospitalini lakini alifariki muda mfupi kabla ya kupatiwa huduma.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kuwepo tukio hilo.
Alisema mtuhumiwa huyo hajafahamika
majina yake na mwili wake umehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia
maiti cha Hospitali ya Rufaa ya KCMC
CHANZO:HABARILEO