MISA YA WANAJESHI WA AFRIKA KUSINI WALIOUWAWA "CAR"

 
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma alihudhuria misa mjini Pretoria kwa ajili ya wanajeshi kumi na watatu wa nchi hiyo waliouwawa katika mapinduzi ya serikali hivi majuzi katika Jamhuri ya Afrika ya kati.
Walifariki katika makabiliano na waasi karibu na mji mkuu Bangui.

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimepuuza madai kuwa wanajeshi hao walikuwa wakimlinda rais Francois Bozize, ili kupata kandarasi za madini kwa ajili ya viongozi wakuu wa ANC.

Upinzani unataka uchunguzi rasmi wa madai hayo.
Zuma alisema kuwa wanajeshi hao walifariki wakiwa wanalinda amani na uthabiti wa bara la Afrika zaidi ya wiki moja iliyopita.

Wakati huo huo, Chama tawala cha ANC, kimekanusha madai ya uhusiano wa kibiashara na Jamuhuri ya Afrika ya Kati uliosababisha vifo vya wanajeshi wake 13.

Wanajeshi hao waliuwawa nchini humo mwezi jana wakati waasi walipouteka mji mkuu katika mapinduzi ya kijeshi yaliyomng'oa madarakani rais Francois Bozize.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo