MAZIKO YA WAKILI NYAGA MAWALA KATIKA PICHA NCHINI KENYA

Mwili wa marehemu Nyaga poul Mawalla ukiwa katika kanisa la Kilutheri nchini Kenya usharika wa Uhuru Highway kwa ajili ya misa 
****
Maziko ya Marehemu Nyaga Mawalla, aliyekuwa Mwasisi na Mkurugenzi wa Makampuni ya Mawalla ya Jijini Arusha yamefanyika jana jijini Nairobi Kenya katia Makaburi ya Jumuia ya Langata.

Mapema kabla ya Maziko hayo yaliyohudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali na familia na marafiki ilifanyika Misa ya kumuombea Marehemu katika Kanisa la KKKK, Uhuru Highway. 

Miongoni mwa Viongozi waliohudhuria ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. Batilda Burian, Viongozi wastaafu, Sir. George Kahama, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Wabunge, Mawaziri wanasheria mabalimbali wa ndani na nje ya Tanzania.

Marehemu Nyaga Paul Mawalla alifariki Machi 22, 2013 jijini Nairobi alikokuwaa amelazwa kwa matibabu  Hospitali ya Nairobi.
Mbunge wa Jimbo la Arusha mjini Chadema ni miongoni mwa waombolezaji waliokuwa kanisani nchini Kenya.
Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe,Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Lazaro Nyalandu na Sir George Kahama wakiwa kanisani wakishiriki misa ya maziko ya marehemu Nyaga Mawalla.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya Dkt Batilda Buriani akiwa na mwanasheria maarufu Jijini Arusha anayemiliki kampuni ya uwakili ya Law /Access Advocates Mosses Mahuna wakiwa nje ya kanisa la Lutherani nchini Kenya.
Mbunge wa Jimbo la Simanjiro wilayani Simanjiro mkoani Manyara Christopher Ole Sendeka na Waziri wa zamani wa mambo ya ndani Laurence Marsha wakiwa kanisani nchini Kenya maziko ya marehemu Paul Mawalla

Kiongozi wa Dini wa Kanisa la Kilutheri Kenya la Uhuru Highway akiongoza Mazishi.
 Sir George Kahama na mkewe wakiweka shada la maua katika Kaburi la Marehemu Nyaga Mawalla.

 Familia ya Marehemu Nyaga Mawalla wakiwa wenye simanzi nzito wakati wa Mazishi hayo.
 Jaji Mark bomani naye alikuwa ni miongoni mwa waombolezaji walioshiriki mazishi hayo.
 Baadhi ya jamaa wa karibu wa Marehemu Nyaga ambao ni wabunge wakiweka Shada la Maua
 Mwenyejiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mkewe wakiweka shada la maua
 Wabunge na Mawaziri mbalimbali wa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakiweka mashada ya maua.
 Wanafamilia wakiweka mashada ya maua
 Watoto wa Marehemu Nyaga wakiwa na ndugu zao.
Balozi wa Tanzania nchini Kenya, dk. Batilda Buriani akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Nyaga.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo