POLISI WALIOSIMAMISHWA KAZI WANA KESI YA KUJIBU


kova
Kufuatia hatua ya wizara ya mambo ya ndani kuwasimamisha kazi baadhi ya maafisa wa jeshi la polisi wanaokabiliwa na tuhuma mbalimbali,  jeshi hilo limesema uchunguzi wa awali  uliofanywa na mahakama ya kijeshi  umebaini kuwa askari hao wanahusika na tuhuma dhidi yao. 

Baadhi ya tuhuma hizo ni pamoja na fedha zaidi ya Shilingi milioni 150, zilikamatwa eneo la Kariakoo jijini Dar es salaam na baadae kupotea katika mazingira ya kutatanisha takribani miezi mitatu iliyopita .

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Kamanda wa jeshi la Polisi kanda maalum ya jijini Dar es salaam, Suleiman Kova amesema licha ya kusimamishwa  kazi askari hao, watafikishwa mahakani wakati wowote. 

Juzi waziri wa mambo ya ndani ya nchi Emanuel Nchimbi, alieleza kuwa serikali haitasita kuwachukulia hatua za kinidhamu askari yeyote atakayebainika kufunja sheria na kufanya kazi kinyume cha maadili.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo