Katika kuhakikisha mkoa wa Iringa unajipanga vema kuondokana na baa la
njaa linaloweza kujitokeza, Mkuu wa mkoa huo, Dokta Christina Ishengoma
amewataka wakulima kutumia fursa za mvua zinazoendelea kunyesha kulima,
kupalilia na kupanda mazao yanayostahimili ukame.
Akizungumza katika
mkutano na wananchi wa kata ya Isimani, Dokta Ishengoma amesema kwa
mwaka huu wa kilimo wa 2013 wakulima hawana budi kutumia vizuri hali ya
hewa na mvua ambayo inaendelea kunyesha kwa kuwa karibu maeneo yote ya
mkoa huo yameweza kufikiwa kikamilifu na mvua za kutosha.
Amesema
kinachotakiwa kwa wakulima hao ni kuhakikisha mazao yao wanayapalilia,
wanazingatia kilimo bora kwa mujibu wa mafunzo na maelekezo ya maofisa
ughani ambao wametawanywa mkoa mzima.
Aidha, amewataka maofisa kilimo
na ughani kuhakikisha wanakuwa karibu na wakulima na kutoa elimu kila
wakati na badala ya kukaa maofisini na kusubiria kuitwa
SOURCE:EBONY FM