WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, amesema Jeshi la polisi limewasimamisha kazi,
na kuwafungulia mashtaka ya kijeshi askari wake katika maeneo
mbalimbali nchini kwa kwenda kinyume na kanuni za kijeshi.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Dk Nchimbi, alisema katika kikao cha
Maofisa na Makamishna wa polisi kilichoketi Dodoma havi karibuni
waliazimia kuanza kuchukua hatua za kinidhamu kwa askari wote
watakaokwenda kinyume na kanuni na maadili ya jeshi hilo.
Nchimbi aliwataja
waliosimamishwa na kufunguliwa makosa ya kijeshi ni pamoja na Elis
Mwita, Mrakibu Mwandamizi wa Polisi ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa
Mkoa wa Mbeya, Jacob Kiango, Mrakibu msaidizi wa Polisi, aliyekuwa
msaidizi wa Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Mbeya, na Charles Kinyongo mrakibu
msaidizi wa Polisi ambaye alikuwa mkuu wa kikosi cha kutuza ghasia
Mkoa wa Mbeya.
Dk Nchimbi alisema askari hao
wote wanatuhumiwa kushiriki mchakato wa kutunza na kusafirisha
mihadarati aina ya cocaine, yenye uzito wa kilo 1.9, yaliyokamatwa
katika kituo cha Tunduma, kuthibitishwa na Maofisa wa Malaka ya Mapato
(TRA), kuwa kweli ilikuwa ni mihadarati.
Alisema lakini walipoyaleta kwa
Mkemia Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam, na kufanyiwa chunguzi
ikabainika kuwa haikuwa mihadarati bali ilikuwa ni Chumvi na sukari.
Dk Nchimbi alisema baada ya
taarifa hiyo Kamati ya Mkoa wa Mbeya ikaomba ifanyiwe uchunguzi na
kubaini kuwa kilichopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali sicho
kilichokamatwa, bali kulikuwa na udanganyifu, jambo lililosababisha
wizara iunde tume iliyobaini kuwa wana tuhuma ya kujibu.
“Askari wadogo wakishirikiana na
maofisa wa TRA waliokamata mihadarati hiyo wanajua chumvi na sukari,
hivyo vigogo hao walishiriki katika njama ya kubadilisha”alisema DK
Nchimbi.
Akizungumzaia mgogoro wa Ardhi
kati ya mwekezaji na wanakijiji, Dk Nchimbi alimtaja Mrakibu Mwandamizi
wa Polisi, Peter Mtagi, kuwa amesimamishwa kazi na kufunguliwa mashtaka
ya kijeshi.
Alisema Mtagi ambaye pia alikuwa
Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kagera anatuhumiwa kuwabambikizia kesi
wananchi kuwa majambazi, waliiba kwa kutumia silaha ili wasipatiwe
dhamana baada ya kupokea rushwa.
“Mimi sipendi watu wafanye
vurugu lakini napenda haki itendeke sasa katika hili askari hawa
hawakufuata taratibu na walikuwa wanajua kuwa wananchi wale
walifanyavile baada ya kufanya mkutano wa hadhara na kubaini kuwa
mwekezaji yule hakuwa na haki ya kumiliki ardhi kiasi hekari
4000”alisema.
Dk Nchimbi alisema wakati
wananchi hao wakiwaswaga ng’ombe kuwapeleka kwa Mkuu wa wilaya, lakini
wakiwa njiani walikamatwa na polisi, na wengine walikimbilia Dodoma
kuonana na waziri mwenyewe.
Alisema lakini wakiwa huko,
alipigiwa simu na askari polisi kutoka Kagera na kuelezwa kuwa watu hao
ni majambazi sugu, hata hivyo, Nchimbi aliomba akutane nao, baini kuwa
wananchi hao hawajawahi kuwa majambazi hivyo walisingiziwa tuhuma hizo
kwa makusudi.
Naye Mkuu wa Kituo cha Polisi
wa wilaya ya Serengeti, Paul Mng’ong’o (SSP), amefukuzwa kazi baada ya
kuingia katika Hifadhi ya Mbuga ya Wanyama Serengeti na kupanga njama ya
kuchimba madini aina ya dhahabu kinyume cha sheria, ambapo hivi sasa
amefunguliwa kesi.
Kwa upande mwingine Dk Nchimbi
alisema suala Kamishna Msaidizi Mwandamizi Renatus Chalamila, ambaye
alikuwa anasimamia ajira za jeshi la polisi, anatuhumiwa kwa pamoja na
maofisa wa polisi kujihusisha na vitendo kupokea rushwa na kuwaingiza
vijana wengi katika Chuo cha polisi kilichopo Moshi, kinyume cha
utaratibu.
“Katika tukio hili vijana 95
ambao waliingizwa katika chuo hicho cha askari bila ya kufuata
utaratibu tumechukulia hatua za kuwafukuza chuoni hapo”alisema Dk
Nchimbi
Nchimbi alisema kutokana na cheo
chaka hicho mwenye madaraka ya kumfukuza kazi ni Rais hvyo taarifa hizo
zomefikishwa kwenye mamlaka hiyo ambapo wakati wakisubiri maamuzi
mengine wanawajibika kumpa likizo ya mwzi mmoja.
Katika hatua nyingine Dk
Nchimbi alisema hawezi kuzungumziwa matukio ya kutekwa na kuteswa kwa
Mwenyekiti wa Chama cha Dk Stephen Ulimboka na tuhuma zinazowakabili
polisi kukwapua fuko lililokwa na sh milion 150 wakati wakitaka kuzima
tukio la ujambazi eneo la Kariakoo mwaka jana, Nchimbi alisema, “hayo ni
masuala ambayo bado yako ngazi ya chini mnaweza kumuuliza Kova, sio
lazima yajibiwe na Waziri endapo atashindwa kufanya hivyo basi
nitawajibika kujibu”.