JELA AU FAINI KWA KUCHEKA KWA SAUTI KUBWA


NewsImages/6832834.jpg

Robert Schiavelli

Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Robert Schiavelli (42) amefikishwa kizimbani mjini new york kwa tuhuma za kuchafua hali ya amani na utulivu kwa kucheka kwa sauti kubwa.
Mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Robert Schiavelli (42) amefikishwa kizimbani mjini new york kwa tuhuma za kuchafua hali ya amani na utulivu kwa kucheka kwa sauti kubwa.

Schiavelli ni mkazi wa kitongoji cha Rockville Center katika jimbo la New York nchini Marekani, alisema kamwe hakuwai kufikiria kwamba ipo siku kucheka kwa sauti ya juu kuna weza kumletea matatizo kiasi cha kufikishwa katika vyombo vya sheria.

Schiavelli alikamatwa nyumbani kwake baada ya malalamiko ya majirani zake, Schiavell anasumbuliwa na ulemavu wa mishipa ya fahamu na amekuwa akitumia kucheka kwa sauti ya juu kama mbinu ya kujirinda.

Polisi katika kituoa cha Rockville Center,imempiga faini Schiavelli ya dola 250 au kwenda jela siku 15, kwa kosa la kuvuruga amani wakati wa usiku.

Wakili anayemtetea Schiavelli, bwana Andrew Campanelli amesema kuwa atapambana kwa nguvu zote kuhakikisha mteja wake anatoka jela.
Nifahamishe.com


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo