Katika pitapita zangu leo nimebahatika kupita barabara ya Matamba-Mfumbi ambapo nimekutana na mandhari hii nzuri ya miti ya asili katika eneo hili lililopo tarafa ya Matamba wilayani Makete na ukiangalia vizuri utaona maporomoko marefu ya maji kwa mbali, ambayo yanazidi kuipendezesha wilaya ya Makete, kwa kweli inapendeza sana
wageni karibuni Makete na pia wenyeji wa makete jijengeeni utaratibu wa kutembelea maeneo kama haya ili kujionea mengi, maana utunzaji wa mazingira nao umechangia hali hii ionekane