KURA ZA AWALI ZAPIGWA KUMCHAGUA PAPA MPYA

Makadinali wakielekea kwenye hekalu kwa ajili ya kumchangua Papa mpya.


Makadinali 115 wamekutana Roma, Vartican City kumchagua Papa mpaya na tayari moshi mweusi umeonekana Vartican City kuashiria kwamba bado papa mpya hajachaguliwa.

Kutokana na utaratibu wa kanisa katoliki makadinali hao wanakutana na kupiga kura kumchagua papa mpya na leo kura za awali zimepigwa, lakini hazikutosha. Baada ya makadinali kupiga na kumpata papa mpya moshi mweupe unaonekana kuashiria kwamba papa mpya amepatikana.

Shughuli hiyo imeanza na misa maalum imeandaliwa katika makao makuu ya kanisa hilo Vatican, St. Peter's Basilica. Baada ya misa makadinali wote wenye umri zaidi ya miaka 80 wataingia kwenye hekalu ya Sistine ambako wamepiga kura.

Makadinali hao wamefungiwa ndani ya hekalu hilo, bila kuwa na mawasiliano na mtu yeyote kutoka nje. Katika nyumba hilo makadinali hao wataapishwa na kuweka siri ya matukio yote wakati wa uchaguzi huo. Inaaminiwa kuwa shughuli hiyo huenda ikadumu siku kadhaa.

Papa mtakatifu Benedikt wa kumi na sita aliwashangaza wengi baada ya kutangaza kujiuzulu. Papa huyo amefanyakazi kwa miaka nane. Ni papa wa kwanza kujiuzulu baada ya miaka 600 iliyopita.

Maelfu ya waumini wa madhehebu ya katoliki wamekusanyika leo nje ya kanisa la St. Peter's Basilica, kufuatilia kwa karibu shughuli hiyo muhimu ya kumteua kiongozi mpya wa kanisa hilo. Makadinali waliochaguliwa watapiga kura mara nne kwa siku hadi Papa mpya atakapopatikana.

Katika nchi nyingine maelfu ya waumini wanafuatilia uchaguzi huo kwenye televisheni na kusikiliza katika. www.habarimasai.com itaendelea kukuletea taarifa zaidi.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo