FILAMU ya Love & Power ambayo ndio kazi yake ya mwisho kuigizwa
na msanii wa filamu nguli Bongo marehemu Steven kanumba inatarajiwa
kuingia sokoni baada ya msambazaji wa filamu hiyo kuikamilisha na kusema
kuwa filamu hiyo itanarajiwa kuingia sokoni mwezi wa nne, filamu ya
Love & Power ni kazi ya kipekee kuigizwa na msanii huyo kabla ya
umauti kumfika ni filamu aliyorekodi siku za mwisho kabisa.
Filamu hiyo pia ina historia ya kipekee kwani moja kati ya filamu iliyobeba wahusika wakubwa ambao ni marafiki wa marehemu Kanumba huku Daktari wa familia ya marehemu naye akiwa ameshiriki vema katika filamu hiyo.
Pengine ni filamu inayoweza kuibua hisia za watu wengi kufuatia filamu hiyo kuigizwa na wasanii watatu ambao kwa sasa ni marehemu, wasanii hao ni pamoja marehemu John Stephano, Hussein Mkiety ‘Sharomilionea’, lakini pia kuna msanii mwinge Irene Paul ambaye aliigiza kama mhusika mkuu, marehemu Kanumba alifariki mwaka jana mwezi wanne.
Msanii huyo anakumbukwa na wapenzi wa filamu kwa umahiri wake wa kuigiza na kuwa ni msanii pekee aliyeweza kuitangaza Tanzania kwa njia ya filamu na kuwa mmoja kati ya watu mashuhuri, filamu ya Love & power itasambazwa na Steps Entertainment ya jijini.