MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Wastara Juma
‘Stara’ amesema kuwa baada ya muda mwingi wa mihangaiko ya kuuguza na
hata kumpoteza mumewe anahitaji kupumzika na kujenga akili upya, katika
kulifanya hilo ameamua kwenda kupumzika Uarabuni kwa ajili ya kutuliza
akili na kujipanga upya, akiongea na BLOG HII amesema kwa sasa anahitaji
kupumzika kwa muda.
“Nina safari wiki ijayo na kwenda Uarabuni kwa ajili ya kupumzika
kisha baadae kuangalia nafanyaje kazi katika staili ipi, kwa sasa
itakuwa ngumu kuwepo bila kufanya kazi lakini pia familia imeamua niende
huko kama ni sehemu ya kunifariji zaidi kutokana na kipindi hiki
kigumu,”anasema Stara.
Lakini mwanadada huyo asiye na makuu ameamua kwenda huko kupmzika
kutokana na hali ya filamu ilivyo sasa ambapo watayarishaji wanajikuta
wakikikaa kwa muda mrefu wakisotea kazi zao kutoka pasipo na wakati
maalum, soko la filamu kwa sasa inasemekana ni gumu kuliko ambavyo jamii
inaliona ukiona kazi imetoka sokoni ujue watu wametabika kwa kiwango
kikubwa.
Tunamtakia mapumziko mema na safari yenye Baraka na baadae akirudi
arudi na nguvu mpya kwa ajili ya kuendeleza sanaa yetu Bongo