Na Ibrahim yassin, Kyela
KAMATI ya siasa ya Chama cha Mapinduzi CCM wilayani Kyela
mkoani Mbeya imepinga taarifa ya utekelezaji wa Ilani iiyotekelezwa na serikali
kwa kipindi cha miaka nane iliyowasilishwa na mkuu wa wilaya Kyela Magreth
Malenga
Taarifa hiyo ilikuja kuwachefua wajumbe hao baada ya Diwani wa kata ya Ikolo George
Mwakabumbe kutaka kujua taarifa iliyosomwa ya maji kuwa hali ni nzuri wakati
katika kata za Ikolo na Muungano wananchi wanakunywa maji machafu kwa kutokuwepo maji salama ya bomba kwa zaidi ya miaka 20
mpaka sasa
Alisema taarifa iliyosomwa na mkuu huyo wa wilaya imepikwa
tofauti na ukweli halisi uliopo katika maeneo ya vijiji na kata mbalimbali na
kuhoji kuwa hajui taarifa hizi kazipata wapi wakati watu wanaugua homa za
matumbo kutokana na watu kunywa maji machafu wanayoyachota kwenye mito ya
Kiwira na Songwe
Msuli Mwaijengo mjumbe wa mkutano huo alisema kuwa hali ya
maji wilayani ni janga la Kiwilaya na kuwa wilaya nzima maji bado ni tatizo na kuwa taarifa hiyo ya
mkuu wa wilaya imepikwa na kuwa mambo mengi ni ya uongo kama taarifa za
mapagala,shule za awali zipo 99 wakati hakuna hata moja na kuwa huo ni utani
Alisema taarifa hiyo
imekichefua Chama Cha Mapinduzi na kuwa anaiomba halmashauri hiyo ya CCM
isiipokee kinyume cha hapo hakuna maendeleo ambayo yatafikiwa Kyela na kuwa
hali hiyo inakipa ugumu chama hicho kujinadi kwa Wananchi
Cliford Mwaikinda
mwenyekiti wa kata ya Tenende,alikasirishwa na taarifa ya maendeleo ya
elimu wakati elimu wilayani Kyela imeshuka kiasi cha kutisha na kuwa elimu ya
msingi na ya sekondari ni mbaya na kuwa
taarifa zilizopo katika taarifa ya zinaonyesha kana kwamba ina matumaini wakati
taarifa hiyo ni tofauti na uhalisia
Kaimu meneja wa mamlaka ya maji safi na maji taka Jorum
Mkuyu alikiri wilaya kutokuwa na maji safi na kuwa hilo limetokana na ukosefu wa fedha na fedha zenyewe ni msaada
kutoka katika benki ya dunia ambazo bado hazijafika na kuwa kama hazitafika
bado tatizo la maji litaendelea Kyela
Afisa mipango Clement Kasongo alisema kuwa hivi sasa kwa
kuwa fedha za benki ya dunia zimesimama
wanatumia mapato ya ndani kuhakikisha kuwa wanafanya kwa sehemu kupunguza ukali
wa tatizo la maji lililopo wilayani Kyela
Mkuu wa wilaya kwa upande wake alisema kuwa anashangaa kuona
baadhi ya madiwani wanapingana na taarifa hiyo wakati katika vikao vya kamati
walipitisha hoja hizo
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt,Hunter Mwakifuna
alisema licha ya taarifa hiyo kuwa na mapungufu wameipitisha na kuwapa muda wa
kujirekebisha kwa yale mapungufu yaliyojitokeza na kuwapa onyo watendaji
kufanya vizuri kwenye miradi mbalimbali ili kukipa nafasi ya ushindi
