BAADA YA KENYATA KUSHINDA URAIS WA KENYA, ODINGA KWENDA MAHAKAMANI KUPINGA

Raila Odinga 
Muungano wa CORD wake Raila Odinga umeelezea kuwa unajianda kwenda mahakamani kupinga matokeo ya urais yaliyompa ushindi Uhuru Kenyatta
Raila Odinga, ameambia waandishi wa habari kuwa kuwa matokeo yaliyotolewa na tume hiyo yalikuwa yamehujumiwa hasa baada ya kutokea hitilafu katika mitambo ya elektroniki iliyokuwa inatumiwa katika shughuli hiyo.

Raila amedokeza kuwa muungano wao unajiandaa kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.

Aidha alisema kugoma kwa mitambo hiyo kulichanganya mambo katika shughuli ya kuhesabu kura. Alisema kuwa baada ya kutokea hitilafu, kura alizokuwa amepata katika maeneo bunge ambayo ni ngome zake , ziliongezwa kwa hesabu ya kura za muungano pinzani wa Jubilee.

Mapema wiki hii, wakati shughuli ya kuhesabu kura za urais ilikuwa inafanyika, CORD walielezea malalamishi kuhusu shughuli nzima hasa baada ya kura kuanza kuhesabiwa kwa mikono badala ya mashine.

Lakini mahakama kuu ilitupilia mbali kesi yao ikisema kuwa haina uwezo wa kufanya uamuzi katika kesi hiyo, na kuwa ni mahakama ya juu zaidi pakee inayoweza kusikiliza kesi hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo