Na Elizabeth John
BAADA ya
kutamba na kibao chake cha ‘Kidela’, mkali wa muziki wa kizazi kipya
nchini, Abdukarim Kiba ‘Abdukiba’ amesema anajipanga kuandaa video ya
kazi hiyo.
Mbali na
‘Kidela’ Abdukiba alishawahi kutamba na vibao vyake kama, Kizunguzungu,
Demu sio na nyinginezo ambazo zilimtambulisha na kufanya vizuri katika
tasnia ya muziki huo.
Akizungumza
ijini Dar es Salaam, Abdukiba alisema kwasasa anatarajia kuanza
kutengeneza video ya wimbo huo ambao amemshirikisha kaka yake ambaye pia
ni nyota wa muziki huo, Alikiba.
“Namshukuru
mungu kazi hii imepokelewa vizuri na mashabiki wangu nab ado inaendelea
kufanya vizuri, naomba tu wapenzi wangu wasichoke kunipa sapoti bado
kuna vitu vizuri ambavyo nimewaandalia,” alisema.
Abdukiba
alisema, video hiyo atafanya na mtayarishaji maarufu nchini Adamu Juma,
ambapo yeye ndio ataandaa mazingira ambayo watafanyia kazi hiyo.
