DIWANI MAKETE NA WENZAKE WAGUSHI SAHIHI NA KUJIPATIA ZAIDI YA MILIONI 2

 Jengo la Mahakama ya wilaya ya Makete
Na Riziki Manfred
Watu wawali wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Makete kujibu tuhuma za kugushi sahihi na kuandika mhutasari wa kikao hewa na kuchukua zaidi ya shilingi milioni mbili katika akaunti ya mfuko wa maendeleo wa kata ya Bulongwa wilayani Makete

Akitoa taarifa hiyo kwa wanahabari ofisini kwake mwendesha mashitaka wa Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Bw. Frednandi Nsakuzi amewataja watuhumiwa hao kuwa ni aliyekuwa diwani wa kata ya Bulongwa Estomin Mahenge na mwenzake Edwin Swallo ambaye alikuwa mtendaji wa kijiji cha Bulongwa ambapo mpaka anafanya tukio hilo alikuwa anakaimu ofisi ya mtendaji wa kata ya Bulongwa 

Watuhumiwa hao waligushi sahihi na kuandika mhutasari wa kikao hewa na kwenda katika benki ya Nmb tawi la Makete na kuchukua zaidi ya shilingi millioni mbili kwenye akaunti ya mfuko wa maendeleao ya kata ya Bulongwa wakidai kuwa ni kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari Usililo ambapo  mhutasari huo upo TAKUKURU

Watuhumiwa hao walifikishwa mahakamani  hapo jana  kwa tuhuma hizo na walikana mashitaka yanayowakabili ambapo kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Machi 23 mwaka huu katika mahakama wilaya Makete na watuhumiwa hao wapo nje kwa dhamana
  
Aidha katika hatua nyingine mkuu wa TAKUKURU wilayani Makete Bwana Daudi Ndyamukama amewaasa wanamakete kushirikiana na taasisi hiyo pindi wanapokuwa na kesi kama hizo hususani inapokuwa katika hatua ya ushaidi mahakamani 

Bw Ndyamukama amesema kumekuwa na vitendo kama hivyo katika vijiji vingi wilayani hapa lakini wananchi wamekuwea hawatoi ushirikiano katika kesi hizo pindi wanapohitajika kutoa ushahidi mahakamani na baadhi yao wamekuwa wakirubuniwa na watuhumiwa


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo