TANZANIA YASAINI MKATABA WA BILIONI 90 KWA AJILI YA MAJI HAPA NCHINI

 (Picha na Issa Michuzi)

Wizara ya Maji imesaini mikataba ya upanuzi wa miradi ya maji katika mikoa ya Kigoma, Lindi na Halmashauri ya mji wa Sumbawanga, makubaliano hayo yaliyofanywa kati ya wizara na Wakandarasi watano.
 
Akisaini mikataba hiyo jana Makao Makuu ya Wizara Ubungo , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Chistopher Sayi aliwataka wakandarasi hao kutekeleza miradi hiyo kwa wakati kama mikataba inavyoeleza.

“Natumia nafasi hii kupongeza wakandarasi wote walioshinda zabuni za kutekeleza miradi hii, lakini pia ni mategemeo yangu miradi yote itafanywa kwa wakati kama ambavyo tumekubaliana katika mikataba hii”. Alisema Mhandisi Sayi.

Wakandarasi waliopata fursa ya kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo ni Spencon Services Ltd ambao watahusika na usambazaji na mifumo ya majisafi mkoani Kigoma; Jandu Plumbers na Metito Overseas watahusika na uchimbaji wa visima katika Halmashauri ya mji wa Sumbawanga.

Jandu Plumbers na Metito Overseas watahusika na uchimbaji wa visima mkoani Lindi na Technofab-Gammon Joint usambazaji na mifumo ya majisafi katika Halmashauri ya mji wa Sumbawanga, na Overseas Infrastructure Alliance watahusika na usambazaji wa maji na mifumo ya majisafi mkoani Lindi.
 
Miradi hiyo ambayo itagharimu takriban shilingi bilioni 90 za kitanzania ambayo imefadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Serikali ya Ujerumani.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo