Mrembo
aliyewahi kupamba video kadhaa za wasanii wa Bongo Fleva ukiwemo
wimbo wa Kidato Kimoja ulioimbwa na J.I, anayekwenda kwa jina la Maya
Silemwe, amedaiwa kumtelekeza mwanaye wa kumzaa aitwaye Junior Justine
(3).
Tukio
hilo la kusikitisha lilitokea hivi karibuni katika kituo cha mabasi
yaendayo mikoani, Ubungo jijini Dar es Salaam ambapo mtoto huyo
aliokolewa na msamaria mwema.
Akisimulia mkasa mzima ulivyokuwa, shangazi wa mtoto huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Monalisa, alisema wao kama familia wameumizwa sana na kitendo kilichofanywa na Maya.
“Maya
amezaa na kaka yangu Justine anayeishi Marekani na amekuwa akimjali
sana kwa kumtumia fedha za matumizi mara kwa mara. Kisa ni kwamba kaka
alimwambia Maya ampeleke mtoto Bukoba (nyumbani kwa baba wa mtoto)
akasalimie, Maya akakubali lakini akamwambia atapitia kwanza Arusha
(nyumbani kwao) ndipo waende Bukoba.
“Justine
akamuelewa lakini kumbe alidanganya, hakwenda Arusha na kuna watu
walimuona akiingia kwenye klabu moja hapahapa Dar es Salaam,
wakamjulisha kaka. Sasa alipompigia kumuuliza, akawa anajing’atang’ata,
siku iliyofuata akadamkia Ubungo ili kumsafirisha mtoto kwenda Bukoba
kwa mama yetu (bibi wa mtoto) lakini alitaka kumsafirisha kwa kumtumia
kondakta,”
alisema Monalisa na kuongeza: “Alikubaliana
na kondakta huyo kisha akamwachia namba ya simu ya mama na yake ili
waweze kuwasiliana na kumpokea mtoto huko Bukoba.
Kwa
bahati mbaya siku ile yule konda alikuwa hasafiri mpaka siku
inayofuatia. Mtoto akaanza kuhangaika stendi siku nzima bila uangalizi
mzuri.
“Bahati
nzuri mama mmoja msamaria mwema akafuatilia na kuonana na huyo konda,
akamuomba namba za mama wa Bukoba kisha akawasiliana naye, kwa kuwa
alikuwa na safari ya kwenda huko siku iliyofuata, akaamua kuchukua
jukumu la kusafiri naye.”
Monalisa
alikubali kutoa namba za simu za msamaria aliyejitolea kusafiri na
mtoto huyo, alipopigiwa alikiri lakini aliomba sana asitajwe .
“Mimi
kama mzazi iliniuma sana kumuona mtoto mdogo anahangaika stendi bila
uangalizi. Nilishangaa sana kuona mzazi aliyeingia ‘leba’ anawezaje
kumwacha mwanaye mdogo namna ile asafiri mwenyewe?” alisema.
baba mzazi wa mtoto huyo, Justine aishiye Marekani ambapo alisema: “Jambo hilo limeniumiza sana. Kwa kweli kama ningekuwa huko nyumbani (Bongo) ningehakikisha namfundisha adabu huyo mwanamke kupitia sheria. “Nashukuru kusikia kwamba mwanangu alifikishwa salama Bukoba.”
Mama wa mtoto huyo alipopigiwa simu alizua kioja baada ya kukataa kwamba hajawahi kumuacha mtoto kwa konda Ubungo na pia akadai eti hana mtoto na wala hajawahi kuzaa katika maisha yake yote. Wakati tukijiandaa kwenda mitamboni juzi Jumatatu, habari zilizopenyeza katika chumba chetu cha habari zilisema kwamba mrembo huyo alimpigia simu mama mkwe wake na kumchimba mkwara mzito.
chanzo:GPL