Kamanda Diwani RPC Mbeya |
WILAYA YA RUNGWE- JALADA LA UCHUNGUZI.
MNAMO TAREHE 25.02.2013 MAJIRA YA
SAA 20:40HRS HUKO KATIKA BENKI YA NMB TAWI LA TUKUYU LILILOPO TUKUYU MJINI
WILAYA YA RUNGWE MKOA WA MBEYA. POLISI WILAYA YA RUNGWE WALIWAKAMATA. 1. JUMANNE S/O MAGERE, MIAKA 29,
MFANYABIASHARA YA DUKA MKAZI WA MLOWO – MBOZI 2. JUMA S/O KABYELO, MIAKA 20, MJALUO, MFANYABIASHARA YA DUKA,
MKAZI WA MSASANI- TUKUYU 3. JOSEPH
S/O PETTER, MIAKA 20, MKURYA, MKULIMA, MKAZI WA MSASANI- TUKUYU NA 4. MIRAJI S/O KETAHA,MIAKA
34,MFANYABIASHARA YA DUKA MKAZI WA
MSASANI-TUKUYU WAKIWA NA KADI 150 ZA ATM ZA WATU MBALIMBALI WAKIWEMO WATUMISHI
WA SERIKALI AMBAPO TAYARI WALIKUWA
WAMESHATOA KIASI CHA TSHS 20,543,000/= KUTOKA KATIKA MASHINE YA ATM .
BAADA YA
KUHOJIWA MTUHUMIWA JUMANNE S/O
MAGERE ANAKIRI KUWASHIRIKISHA WATUHUMIWA WENZAKE KUMSAIDIA KUTOA KIASI HICHO
CHA PESA NA KWAMBA KADI HIZO NI MALI YA WATEJA WAKE AMBAO WENGI NI WILAYA YA MBOZI WALIOKOPA VITU MBALIMBALI KATIKA
DUKA LAKE ANALOUZA BIDHAA ZINAZOTUMIA UMEME ZIKIWEMO REDIO,TELEVISION PIA
VYEREHANI,MAGODORO NA BAISKELI NA KUWA WATEJA WAKE NDIO WALIOMPATIA KADI HIZO
PAMOJA NA NAMBA ZAO ZA SIRI [PASSWORD] ILI AWEZE KUKATA DENI ANALOWADAI NA
KUWAPATIA KIASI CHA PESA KINACHOSALIA.
KUFUATIA TUKIO HILO WATUHUMIWA WAMEENDELEA KUHOJIWA KITUO CHA POLISI
TUKUYU-RUNGWE WAKATI PIA UFUATILIAJI UKIFANYWA KWA WENYE KADI HIZO ZA ATM. UFUATILIAJI UNAFANYWA PIA KUONA KAMA KUNA UKOPESHAJI WA FEDHA
TASLIMU UNAOHITAJI MALIPO NA RIBA ILI HATUA ZINAZOSTAHILI KISHERIA ZIWEZE
KUFUATWA. HADI SASA UCHUNGUZI HAUJABAINI WIZI WA MOJA KWA MOJA ULIOFANYWA NA
WATUHUMIWA KAMA ILIVYORIPOTIWA NA BAADHI YA VYOMBO VYA HABARI WALA HAKUNA
TAARIFA YA MTU KUIBIWA KWENYE AKAUNTI YAKE.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA
MBEYA KAMISHNA MSAIDIZI WA
POLISI DIWANI ATHUMANI ANATOA WITO KWA WANANCHI
KUWA MAKINI SANA NA “TRANSACTIONS” ZINAZOHUSU AKAUNTI ZAO KWA KUWA KUMEKUWA NA
MALALAMIKO KADHAA YANAYOFIKISHWA VITUO VYA POLISI LAKINI YAKIFUATILIWA INABAINIKA
KUWA CHANZO NI UTOAJI HOLELA WA NAMBA YA SIRI YA MWENYE AKAUNTI.
Signed By,
[DIWANI ATHUMANI - ACP]
KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA.