Kamanda Charles Kenyela
Jeshi
la Polisi mkoa wa Kinondoni Jijini Dar es Salaam limefanikiwa
kuwakamata majambazi sugu 21 kufuatia doria na misako mikali
inayoendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kinondoni.
Akitoa
taarifa kwa vyombo vya habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni
Charles Kenyela (Pichani) amesema kumatwa kwa majambazi hayo kunatokana
na ushirikiano mzuri baina ya wananchi na Jeshi la Polisi kwa njia ya
kutoa taarifa zenye uhakika kuhusu uhalifu na wahalifu kwenye maeneo
yao.
Katika
tukio jingine Kamanda Kenyela amesema jambazi sugu ajulikanaye kwa jina
la Omary Said mwenye umri wa miaka 37 mkazi wa Tabata Aroma amefariki
dunia kufuatia kipigo kikali alichokipata kutoka kwa wananchi wenye
hasira kali baada ya yeye na wenzake watatu waliotoroka baada ya tukio
la kumvamia Abdulrahaman Mohamed na kumpora pesa taslimu Tshs.
14,000,000/= zilizokuwa kwenye mfuko wa Rambo.
Aidha
Jeshi hilo la Polisi Mkoani Kinondoni huko Kimara Temboni limefanikiwa
kukamata silaha moja aina ya S/Gun yenye namba T 23269 na risasi 20
zilizokuwa kwenye mfuko wa Rambo baada ya majambazi wawili waliokuwa
wanajiandaa kwenda kufanya uhalifu maeneo ya Kimara Temboni kuwa
walikuwa wanafuatiliwa na askari na hatimaye kuamua kuitupa silaha hiyo
na risasi zake.