Mwalimu mmoja wa shule ya
sekondari ya kata ya Kitulo wilayani Makete aliyefahamika kwa jina la Casto Sote Kawamba ameuawa kwa kupigwa risasi na askari wa jeshi la
polisi Makete
Akizungumza na mwandishi wa mtandao
huu ofisini kwake mkuu wa polisi wilaya ya Makete SP Peter Kaiza amesema tukio
hilo lililotokea eneo la benki ya NMB tawi la Makete siku ya jana majira ya saa
moja na robo usiku na kuongeza kuwa mwalimu huyo alikuwa anakwenda kupata huduma za kibenki
kupitia ATM akiwa na pikipiki ndipo alipo amriwa na askari mmoja aitwaye
Jose Msukuma na kudai kuwa alikuwa hajavaa kofia ngumu ya kuendesha pikipiki (helment) na
alipoamriwa kusimama alikaidi amri hiyo na kutaka kumgonga askari huyo aliye kuwa
lindokatika benki hiyo
Kaiza amesema ndipo askari huyo katika kujihami alifyatua risasi zilizopelekea kifo cha mwalimu huyo
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya Makete Bw, Idd Nganya ambaye ni mwajiri wa marehemu
amesema kuwa amepokea kwa majonzi makubwa taarifa za kifo cha mtumishi wake na kusema taarifa alizonazo ni kwamba mwili wa marehemu bado umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Makete wakati utaratibu wakusafirisha mwili huo
kwenda nyumbani kwa marehemu huko Mbeya kwa ajili ya maziko ukiendelea
Baadhi ya
walimu wenzake na marehemu ambao walifika hospitali kujua kuhusina na kifo cha
mwalimu mwenzao wamelaani tukio hilo na kusema kuwa nilakikatili
na linapaswa kukemewa kwa nguvu zote
Mganga mkuu mfawidhi wilaya ya Makete Dkt. Michael Gulaka amesema
kuwa wao walipokea mwili wa marehemu na sio akiwa majeruhi
Mtuhumiwa wa mauaji hayo tayari anashikiliwa na jeshi hilo
ONYO: PICHA ZA TUKIO HILI ZINATISHA, KAMA HUPENDI KUZIONA TAFADHALI USIENDELEE CHINI