![]() |
| Dk Shukuru Kawambwa. |
Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa amesema kwamba
matokeo ya kidato cha nne yatatangazwa wiki hii kufuatia swali
aliloulizwa kutaka kujua ni lini matokeo hayo yatatangazwa.
Dk Kawambwa alitangaza hilo pamoja na ajira mpya za walimu alipokutana na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam.
Kufuatia kauli ya Waziri huyo, inamaana sasa matokeo hayo yatatangazwa si zaidi ya kesho (Ijumaa) hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba siku za kazi kwa ofisi za serikali zinaishia Ijumaa.
Alisema serikali haijachelewa kutangaza matokeo hayo kwani wanafunzi watajiunga na kidato cha tano Julai mwaka huu. “Hapo mtasema tumechelewa kivipi?
