MAHAKAMA YAMHUKUMU BOBBY BROWN KIFUNGO CHA SIKU 55

Bobby Brown amehukumiwa kutumikia kifungo cha siku 55 ndani
ya jela ya Los Angeles na miaka minne ya matazamio, baada ya kupatikana na
hatia ya kuendesha gari akiwa amelewa na pia leseni yake ikiwa  imezuiwa. 

Hukumu hiyo imetolewa jana February 26 na mahakama ya L.A, na pia mahakama hiyo imetoa amri kuwa Brown anatakiwa kuhudhuria program ya matibabu ya ulevi uliopitiliza kwa muda wa miezi 18.

Mwanasheria wa jiji hilo Frank Mateljan amesema mwimbaji huyo amehukumiwa kifungo hicho baada ya ushahidi wa kutosha unaoonesha aliakuwa anatumia leseni iliyozuiwa kuendelea kutumika.

B. Brown anatakiwa kuripoti kwenye jela ya Los Angeles kabla
ya March 30 mwaka huu.

Mme huyo wa zamani wa marehemu Whitney Houston alisimamishwa
na polisi akiwa anaendesha gari lake kwa mwendo wa hatari October, 2012, na
baadae polisi waligundua gari zima lilikuwa limebeba vilevi na yeye mwenyewe
amekunywa. 

Brown alishawahi kukamatwa mara mbili kwa makosa kama hayo,
mwaka 1996 na mwaka 2012, na leseni yake ilisimamishwa kutumika tangu mwaka jana baada ya kukutwa na makosa hayo.

Bobby Brown alimuoa marehemu Whitney Houston kwa miaka 15 na
baadae wakaachana mwaka 2006. Brown na Whitney walibarikiwa kupata mtoto mmoja tu wa kike ‘Bobbi Kristina Brown’ ambae alizaliwa March 4, 1993.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo