MKONGWE katika filamu Bongo, Richard Mshanga ‘Masinde’ ameonesha makali yake baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo iliyokuwa ikishikiliwa na kinara anayesumbua soko kwa sasa, Jacob Steven ‘JB’ au Bonge la Bwana.
Masinde ambaye awali aling’ara na Kundi la Shirikisho Msanii Afrika la jijini Dar es Salaam, ametwaa Tuzo ya Msanii Bora wa Kiume (2012 – 2013) iliyotolewa na Zanzibar Film Festival ‘ZIFF’ ambayo mwaka uliopita ilikuwa inashikiliwa na JB.
Akipiga stori na Mwanahabari, Masinde alisema: “Siwezi kusema kwamba mimi ni bora kuliko JB ila nashukuru kuona kwamba kazi zangu zinathaminiwa na hatimaye nimepata tuzo hii.
“Kwa kweli imenipa moyo na itanisukuma kufanya kazi bora zaidi hasa kipindi hiki ninacho tayarisha filamu zangu.