![]() |
| Silaha haramu zikiteketea baada ya kuchomwa moto. Imeelezwa kuna zaidi ya silaha haramu 500,000 katika nchi zilizomo ndani ya Jumuiya ya Afrika Mashariki. |
Na Dotto Mwaibale
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania Dk.Mohammed Gharib Bilal amesema mogogoro mbalimbali
iliyopo katika za Jumuiya ya Mashariki inachangiwa na kuwepo kwa silaha
haramu katika nchi hizo.
Hayo aliyasema Dar es Salaam leo
katika zoezi la uteketezaji wa silaha haramu lililofanyika Ukonga
Magereza na kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa jumuiya hiyo.
"Takwimu zilizopo zimebaini kuwepo
kwa silaha ndogo ndogo na kubwa ambazo hazimilikiwi kihalali na
kusababisha kuwepo kwa matukio mengi ya kihalifu" alisema Bilal.
Alisema katika ukanda wa Afrika
Mashariki takwimu zinaonesha kuna kuwepo kwa silaha haramu 500,000 hali
inayoonesha kuwa kuna kazi kubwa katika kukabiliana na migogoro na aina
mbalimbali za uhalifu katika jamii yetu.
Aliongeza kuwa katika ukanda huo
kumekuwa na ongezeko la matukio ya kihalifu yanyotumia silaha na
yamekuwa yakitokea maeneo ya mipakani na yale yanayohusisha muingiliano
wa watu kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Bilal alibainisha kuwa matukio ya
ujambazi, uvamizi na mengine ya aina hiyo yamekuwa yakiongezeka na
chanzo chake ni kuwa na raia wasio waaminifu hasa wale wanaomiliki
silaha haramu.
Alisema athari ya wazi kabisa
inayotokana na ongezeko la silahaaaa haramu ni ile inayojitokeza katika
Sekta ya Utalii ambako tunashuhudia kuongezeka kwa matukio ya ujangili,
ivamiziunaofanywa na maajangili katika mbuga za wanyama na kuhatarisha
kwa kiasi kikubwa katika sekta hiyo.
Dk. Bilal alitumia fursa hiyo
kuishukuru Serikali ya Ujerumani kupitia Balozi wake hapa nchini H.E.
Klaus-Peter Brandes kwa kuisaidia jumuiya ya Afrika Mashariki
kukabiliana na tatizo la silaha haramu kupitia shirika la Maendeleo la
GIZ ambalo limesaidia kufanya zoezi hilo la kuteketeza silaha hizo.
"Nineambiwa kupitia ushirikiano kati
ya Jumuiya yetu na GIZ masuala mbalimbali yamefanyika ambapo baadhi ya
hayo ni kuijengea uwezo sekretarieti ya Jumuiya na nchi wanachama kwa
kuratibu utekelezaji wa mpango wa kupambana na silaha haramu" alisema
Dk. Bilal.
Dk. Bilal alizitaka nchi za Jumuiya
ya Afrika Mashariki kuungana katika kukabiliana na ongezeko la silaha
haramu haraka iwezekavyo bila ya kusubiri kwani jukumu la ulinzi ni la
nchi zote zilizopo ndani ya jumuiya hiyo.
Balozi wa Ujeruman nchini H.E.
Klaus-Peter Brandes, alisema matumizi ya silaha za maangamizi ni moja ya
madhara ya mradi wa EA katika kukabiliana na SALW kwenye ukanda wa
Afrika Mashariki ambao miaka sita iliyopita aliishauri sekretarieti ya
Afrika Mashariki kukaa pamoja na serikali zao kuzungumzia suala hilo la
kuzagaa kwa silaha hizo haramu.

