MAMBA ALA MTU MKOANI NJOMBE

MTU mmoja Ernest Fabiani Mahundi (56) mkazi wa kijiji cha Kiyogo Masasi Wilayani Ludewa katika Mkoa wa Njombe ameuwa na mamba na kisha kumtafuna mwili wake na kubakiza miguu peke yake.

Kwa mujibu wa afisa mtendaji wa kijiji cha Kiyogo Samweli Gama februari 10 mwaka huu marehemu Ernest Mahundi alivuka mto Luhuhu na kwenda katika kitongoji cha Lukali kilichopo kijiji cha Ngingama wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma kwa ajili ya kunywa pombe kama ilivyodesturi na alipokuwa akirudi akapatwa na mkasa huo.

Afisa mtendaji huyo akaongeza kuwa baada ya kugundua kupotea kwa marehemu aliitisha wananchi na kuanza kumsaka akiwa hai au amekufa na msako huo nulidumu kwa muda wa  siku mbili ambapo kiwiliwili cha marehemu kilipatikana maeneo ya kijiji cha ngelenge (fokland) kwenye kisiwa cha wavuvi akiwa ameliwa mwili wote na Mamba na kubakizwa miguu na kiuno huku kikiwa na suruali.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo