Na Ibrahim Yassin,Mbeya
WAFANYABIASHARA wa soko kuu la Kyela mkoani Mbeya
wamelalamikia kitendo cha soko hilo
kutokuwa na huduma ya choo kwa muda wa mwezi mmoja sasa baada ya kilichopo
kujaa
Akizungumza kwa niaba ya
wafanyabiashara wa soko hilo Hussein Taidin (Saddam) alisema kuwa soko
hilo limekosa huduma hiyo
kwa muda sasa kiasi kwamba baadhi yao wanajisaidia kwenyemifuko laini
(rambo) na kutupia kwenye mapipa ya taka taka licha ya kuwa ushuru wa
soko wanatoa kila siku
Alisema hivi sasa wao wanakwenda umbali mrefu sana kwenda kufuata huduma
hiyo ya choo kwa kulipia na kuwa muda mwingi unapotea kwa kwenda mbali na kuwa
hawaoni sababu za kufanya choo hicho kisiendelee kutumika wakati fedha zipo na
zinaendelea kutolewa na wafanyabiashara
Amedai kuwa wao wamekuwa wakionana na kuwasilisha kero hiyo
kwa viongozi wa soko lakini wamekuwa hawapati majibu ya kuridhisha kiasi cha
kuomba msaada kwenye vyombo vya habari
Katibu msaidizi wa soko hilo Philimoni Mahenge alikiri
kutokuwepo kwa huduma hiyo katika soko kwa muda wa mwezi na zaidi na kuwa hiyo
imetokana na choo hicho kujaa na jitihada za kunyonya uchafu ndani ya choo
hicho unaendelea
Alisema kuwa uongozi wa soko kwa kushirikiana na mamlaka ya
mji mdogo wa Kyela wamekuwa wakifanya jitihada za kukodi gari za kunyonya maji
machafu na kuwa gari hilo lipo moja mkoa mzima hivyo inakuwa ngumu gari hilo kufika kwa wakati
pale linapohitajika
Mkuu wa wilaya Kyela Magreth Malenga kwa upande wake
alisema kuwa ofisi yake imepata taarifa hizo kuwa anachokifanya ni kusaidia
kuwezesha kupatikanika kwa huduma hiyo haraka na wafanyabiashara wakaendelea
kukitumia choo hicho