Na Ibrahim Yassin,Kyela
MWANAFUNZI wa darasa la sita katika shule ya msingi ya
Kasumulu kata ya Ngana wilayani Kyela Kaselema Mpale (14) wa ameuawa kikatili
kwa kuchinjwa na kisu kisha kunyofolewa baadhi ya viungo sehemu za mwili wake
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi mama wa mtoto huyo Lucia Kamnyonge
alisema kuwa tukio hilo lilitokea siku ya Ijumaa ambapo mnamo majira ya saa
10;30 baba yake alimtuma mtoto kwenda nyumba ya jirani kuchukua mpunga ambao
ungetumika kama chakula cha siku hiyo
Alisema kuwa toka siku hiyo alipotumwa mpunga akuweza kupatikanika hadi alipokutwa
siku ya pili yake akiwa amekufa kwa kuchinjwa na kisu na na kunyofolewa baadhi
ya sehemu zake za mwili ambazo ni Pua,mdomo,jicho ,kuondolewa sehemu zake za
siri na kuchunwa ngozi ya kichwa karibu na utosi na mwili wake kutundikwa juu
ya mti
Amefafanua kuwa baada ya hali hiyo kujitokeza taarifa
ilipelekwa kwenye ofisi ya serikali ya kijiji ambapo uliitishwa mkutano wa
wananchi wote wa kijiji hicho na ndipo wote walipotawanyika kuanza kumtafuta mtoto huyo bila ya mafanikio baada
baba yake alipomkuta mtoto huyo juu ya mti akiwa ametundikwa kichwa chini miguu
juu na viungo vyake hivyo vikiwa vimenyofolewa
Mwenyekiti wa kitongoji cha Ibungumbati katika kijiji hicho cha Ushrika lilipotokea tukio
hilo ,Adamu Mkese alisema kuwa tukio hilo imeweza kuwashitua watu wa eneo
hilo na kuwa katika mkutano wa kijiji
uliokaa kwa dharura wananchi walimuhusisha baba mzazi wa mtoto huyo ,Mpale
Mbisa (35) kuhusika katika mauaji ya mtoto huyo
Alisema kuwa watu wa kijiji hicho wamemuhusisha baba wa
mtoto huyo kutokana na mazingira ya kifo chenyewe na maelezo ya kujichanganya
anayoyatoa baba huyo wa mtoto hasa jinsi yeye alivyomkuta mtoto huyo akiwa
amekufa licha ya jamii ya watu wa eneo hilo kumtafuta mtoto huyo mchana na
usiku bila ya kumuona na kushangazwa na taarifa kuwa yeye amemuona tena
kiurahisi zaidi tena maeneo ambayo watu wote walipita kumtafuta mtoto huyo
Mwenyekiti huyo wa kitongoji
alisema kuwa katika mkutano huo wa kijiji mambo mengi yalizungumzwa na kuwa
mzazi huyo wa mtoto alichukua fedha kwa mtu kiasi kama shs,milioni 7 ili
kumuuza mtoto wake huyo ambapo alitekeeza azma hiyo na kulazimika kumkamata na
kumpeleka polisi ambako bado anashikiriwa
Ofisa mtendaji wa kijiji hicho cha Ushirika ,Naomi Charles alisema kuwa kuna dalili zote za baba
huyo wa mtoto kuhusika katika mauaji
hayo kutokana na mazingira na kujichanganya kwa maelezo anayoyatoa na kuwa bado
kuna watu wengine watatu ambao wanahusishwa na mauaji hayo na kuwa polisi
wanaendelea na uchunguzi zaidi
Alisema hisia hizo za
wananchi zinaweza kuwa na ukweli ndani yake na kuwa jeshi la polisi linabidi
kufanya uchunguzi wa kina na kuwa kama ataachiwa usalama wake utakua mdogo pale
kijijini kutokana na watu walivyo na hasira naye kufuatia tukio hilo
Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Ushirika Baruti Mwakasala
alisema kuwa hari katika kijiji hicho si nzuri na kulishukuru jeshi la polisi
kwa hatua za haraka walizozichukua na kuwa baada ya uchunguzi polisi waliruhusu
mwili wa Mwanafunzi huyo kuzikwa
Alisema hisia za wananchi juu ya tukio hilo si za kubezwa na
kuwa polisi wamepata pa kuanzia katka kufanya uchunguzi wao na kuwa ukweli
utabainika tu
Ofisa tarafa wa tarafa ya Unyakyusa,Lwitiko Mwakalukwa
alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa yeye na mkuu wa wilaya walifika
eneo la tukio na kujionea unyama huo na kutoa maagizo kwa jeshi la polisi kufanya uchunguzi wa kina na wa
haraka ili watu waliofanya kitendo hicho wabainike na kufikishwa mbele ya
vyombo vya sheria