UKOSEFU WA ELIMU YA BARABARANI BADO TATIZO KWA MADEREVA BODABODA

 
Imesemekana kuwa tatizo lililopo wilaya ya Hanang’ Mkoania Manyara kwa upande wa boda boda ni elimu hawapewi kuhusu sheria za barabarani hivyo wanatakiwa kufuata sheria na kanuni za barabarani kuweza kupunguza vifo vya wanaboda boda.
 
Hayo yamesemwa na mkuu wa polisi wilaya ya Hanang’ Arute Makita wakati akitoa maoni yake kwenye kikao cha watumishi wa idara mbalimbali kilichofanyika wilayani humo mkoani Manyara.
 
Aliongeza kuwa ili kuweza kupunguza tatizo la ajali za waendesha pikipiki yaani boda boda barabarani wamiliki wao pamoja na waajiri wao wanatakiwa kuwapeleka shule ili kuweza kupata elimu ya kutosha ili kuweza kupunguza vifo vya ajali vinavyotokea wakati wanapoendesha boda boda hizo.
 
Alibainisha kuwa tangu mwezi wa sita mwaka jana mpaka sasa januari mwaka huu zaidi ya watu 23 wamekufa kwa boda boda hivyo waendesha boda boda wanatakiwa kupatiwa elimu ya kutosha ili kuweza kupunguza vifo vya boda boda.
 
Naye mwakilishi kutoka mahakama ambaye ni hakimu mhifadhi wilaya ya Hanang’ Saidi Ding’ohi amewataka watumishi nchini wafanye kazi kwa bidii na kuzingatia sheria na kanuni za kazi nakuweza kuzijua .
 
Pia amewataka washiriki wa kikao hicho ambao ni watumishi wa idara mbali mbali kuhudhuria siku ya sheria itakayofanyika mwanzoni mwa mwezi wa pili nchini kote ili kuweza kujua kanuni na sheria za kazi.
 
Kwa upande wake kutoka idara ya kilimo Afisa umwagiliaji Phineas Kasasi alisema kuwa ili kuweza kwenda mbele bajeti ya kilimo kuhusu pembejeo zinatakiwa ziwafikie kwa wakti wakulima na elimu inatakiwa itolewe ya kutosha kwa wakulima.
 
Aidha aliendela kusema kuwa wanaofanya kazi watu wa vijijini wanatakiwa kupewa kipaumbele pia miradi mbali mbali imeingiliwa na wanasiasa ambapo wanataka wao kuiongoza au kuisimamia wao wametakiwa kuacha tabia hiyo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo